DIS Vs Academic Inter. School

DIS Vs Academic Inter. School

BelindaJacob

Platinum Member
Joined
Nov 24, 2008
Posts
6,474
Reaction score
4,039
Habari wapendwa,

Naomba wazazi mnisaidie kuniambia kati ya Dar-es-saalam Independent School (DIS) na Academic International School, ipi ni shule nzuri kitaaluma na mambo mengine muhimu kuzingatia katika kumjenga mtoto pia reputation ya shule? Shule zote zipo maeneo ya mikocheni. Nadhani hawatumii curiculuum ya Tanzania. (correct me kama nimekosea)

Nipo njia panda kwa mtoto kujiunga kati ya hizo mbili kwa darasa la 1..Naelewa pia ukiacha yote nafasi ya mzazi kumlea mtoto kimaadili mema na kufuatilia maendeleo yake ya shule iko pale pale.

Asanteni!!
 
Nami nilikuwa natafuta sana kujua maana tujiandae kwa watoto wetu angalau wapate elimu fulani ambayo sisi tuliikosa sababu ya umasikini labda na kutokuwepo shule hizo wakati wetu!!
 
Asante Skills4Ever.. ni muhimu sana kujipanga na haya mambo kuhusu watoto wetu. kwa kuanzia inabidi uchukue application forms katika shule zote na hapo unapata info. kadhaa kuhusu ada, ratiba ya msimu wa masomo, usafiri nk..


Mkuu Njiwa..nashukuru kwa maoni yako, nilipita pale kuangalia mandhari pia kuonana na mkuu wa dept. ya primary
 
Back
Top Bottom