Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Kulingana na daktari wa afya ya uzazi wa wanawake nchini Tanzania Dkt Berno Mwambe, hali hii kwa Kiingereza hufahamika kama Disorder of Sex Development (DSD). Hii ni hali ya viungo vya uzazi kukosa kukomaa.
Anasema kuna aina nyingine ya ugonjwa unaojulikana kama Mayer-Rokitansky-Kuster-Hauser (MRKH) syndrome, ambao unahusu mwanamke kukosa viungo vyote vya sehemu za uzazi .
Daktari anaongeza kuwa hali hii inatokea mara chache sana kwa watoto wa kike, kwa wastani mtoto 1 Kati ya 4,500 wanaozaliwa.
Hali hii inasababishwa na mabadiliko katika vinasaba vinavyohusika katika ukuaji wa viungo vya mwanamke.
Na je marekebisho yanaweza kufanywa? Dkt Berno anasema kuwa inategemea usugu wa hali yenyewe. Kwa mtu ambaye viungo vyake vya uzazi havijakua vizuri, basi mtu anaweza kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha.
Kwa mtu ambaye hana kabisa kwa mfano Bi Musamba, matibabu yake yanakuwa magumu hususan kwenye muundo na tamaduni za jamii za kiafrika zilivyo.
Aidha daktari anasema kuwa nchi za ng'ambo hufanya marekebisho na hata kumpandikiza mwanamke mji wa uzazi wa mtu mwingine na hata kutengeneza uke. Mwathirika anaweza kufanikiwa hata kushika na kuubeba ujauzito baada ya upasuaji na tiba ya homoni.
Anaitwa Baby John Musamba (26) alizaliwa huku jinsia yake ikiwa haitambuliki (Jinsia Tata) na anaishi na hali hiyo hadi sasa, inawezekana umeshakutana na clip yake akiwa anaomba kura mbele ya Wajumbe, Baby anasema dhamira yake ni kwenda Bungeni ili kuwasemea wenye tatizo kama lake ambao wengi wamekuwa wakijificha au Familia zao kuwaficha.
“Sina jinsia, sipati hisia za kimapenzi, nilikuwa naumizwa sana kuitwa Jike Dume, wenye tatizo kama langu wako wengi lakini wengi wanajificha, nataka kuingia Bungeni nikawasidie, natamani kupata platform, kuanzisha foundation ili kupaza sauti”-Baby John.
Yapo mengi ambayo tumezungumza na Baby John tulipomtembelea nyumbani kwa Kaka yake mbele kidogo ya Fremu kumi Kivule DSM kuhusu maisha aliyopitia tangu anazaliwa hadi sasa.