Jamani wana JF naomba nitoe shule kidogo kuhusu Mradi walioufungua hao ndugu zetu. Kwanza siyo mradi Mgeni hapa nchini na kwingineko Duniani. Ni kitu kinafanyika katika vyuo vikuu vingi na maarufu kuliko vyuo vyetu vya kibongo. Nakubaliana na mawazo kuwa watu wafanye kazi independently ili kujenga umahiri katika fani yoyote ile amabayo mtu anasomea au anayofanyia utafiti.
Lakini tukumbuke kuwa proof reading of dissertation (s) siyo kumfanyia mtu utafiti wala kumwandikia mtu wawazo. Nikuwa mtu anakuwa amekwisha fanya tafiti na ameandika matokeo ya utafiti wake. Ripoti inaweza kuwa kurasa zaidi ya 100! kusoma ripoti nzima wewe mwenyewe kwa maana ya kuupitia upya unaweza usigundue makosa kwa maana mawazo uliyatoa wewe na uliyaandika wewe kwahiyo kugundua makosa siyo rahisi kama vile unyoofu wa sentensi, koma, kituo kikuu na alama nyingine nyingi. Mtu mwingine tofauti na mwandishi ni rahisi kufanya editing kwa namana hiyo.
Kingine nikuwa, proof reading kwa mtu wa Masters na PhD inafanyika kwa mtu ambaye tayari anajua kuwa anataka nini na siyo kweli kuwa kila wazo la proof reader ataikubali. Lazima wata-negotiate namna ya kuweka wazo linaloonekana kuwa linahitaji kuboreshwa katika ripoti. Lakini pia ieleweke kuwa proof reading inasaidia kuokoa muda wa uandishi wa ripoti ya utafiti au kitu chochote kile kama vile articles nk. Niwaulize ninyi mnaobisha kuwepo kwa kazi hii kuwa Wahariri wa Magazeti wanadumaza akili za wanaoandika articles au makala katika magazeti?
Katika masomo ya Sayansi na Hisabati (science and mathematics subjects) kuna matumizi ya calculator, hivi, zinafaa kutumika mashuleni?Hivi, calculator zinadumaza ubongo za wanafunzi wetu Tanzania?Kuna matumizi ya computer katika kufanya mambo mbali mbali hata katika planning, kuchora majengo, kufanya mahesabu nk; hivi, nayo hayafai?
Hebu fikiria hawa watu na mabango yao hapa chini, je wangeenda kwa proof reader haya makosa yangeonekana?
SCOOL ; YOUR WELLCOME; Nk.
Kwaheri wandugu!