DIT B.eng in oil & gas engineering Vs B.sc in Petroleum engineering

D Downstream itoe hapo, downstream sio nyepesi kiivo,
 
Gas ipo ndani ya Petroleum, ukitaka kujua utofauti wa petroleum na oil and gas engineering angalia kozi content
 
Shahada ya uhandisi katika uhandisi wa mafuta na gesi (BE Oil and Gas Engineering) na Shahada ya Sayansi katika uhandisi wa petroli zote ni kitu kimoja.

Kinachoweza kuzitofautisha ni mtaala ambao utatungwa na kufundishwa katika chuo husika.

Lakini unaweza kuamua kufundisha mtaala mmoja.

Wakati mwingine unaweza amua zote zitumie mtaala wa kozi za mkondo wa juu (upstream) au ukaamua zote zitumie mkondo wa chini (downstream) au wakati mwingine ukaamua mojawapo ikatumia mtaala wa kozi za mkondo wa juu na mkondo wa chini.

Kuzitofautisha ni maamuzi ya watunga mtaala ila zote ni kozi moja.

Tunapoanza kutafuta hydrocarbons huwa hatutafuti gesi huwa tunakua na lengo la kutafuta mafuta. Gesi huwa inapatikana kwa bahati mbaya. Na tunapoona mafuta hamna tunaamua kuendelea na gesi.

Hivyo unapotaka kuchagua hizo kozi usiangalie majina. Angalia mtaala wanaotumia.

Kama unataka kuelewa kwa undani mfumo mzima wa mafuta na gesi ardhini na jinsi ya kuchimba na kuzalisha hayo mafuta na gesi ni vyema ukasoma shahada sayansi ya uhandisi wa petroli UDSM.

Kama unataka kuelewa mkondo wa kati kwa kina na kwa mbalii mkondo wa chini. Nenda kasome uhandisi wa mafuta na gesi DIT.

Mwisho wa siku mwaajili akitangaza kazi fulani ataangalia mtaala uliotumia wakati unasoma shahada yako.

Kazi kama ya reservoir engineer inahitaji uwe umeelewa kwelikweli kanuni mbalimbali za reservoir engineering.

Uwe umesoma kozi hizi katika mtaala wako:
1. Geology 1
2. Petroleum geology 1
3. Reservoir fluid properties
4. Reservoir engineering 1
5. Reservoir engineering 2
6. Reservoir simulations: Hapa uwe na uwezo wa kusimulate kwa kutumia MRST, CMG, na ECLIPSE.

Baada ya hapo ndio kuna kozi za
1. Production engineering 1
2. Production engineering 2
3. Drilling engineering 1
4. Drilling engineering 2


Kama mtaala wa shahada mojawapo unagusa vitu hivyo basi hapo utakua unakamilisha kuweza kufanya kazi zote tatu za mkondo wa juu yaani.
1. Mhandisi wa uzalishaji wa gesi au mafuta (Production engineer)
2. Mhandisi wa uchimbaji wa gesi au mafuta (Drilling engineer)
3. Mhandisi wa Reservior
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…