DIT yaanza kuunganisha magari kwenye mfumo wa gesi

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
552
1119962

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeanza kuunganisha magari kwenye mfumo wa matumizi ya gesi asilia badala ya petroli na kwamba hadi sasa magari 150 yamekwishaunganishwa.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge, Mratibu wa Mradi wa Matumizi ya Gesi Asilia kwenye magari (CNG Vehicle Project) kutoka DIT, Dk Esebi Nyari alisema pamoja na idadi hiyo ya magari 150 wanatoa mafunzo zaidi kwa wataalamu kuhusu mfumo huo. Alisema katika kutekeleza mradi huo wanashirikiana na kampuni ya wazawa ya Energo Tanzania Limited ambayo ni kwa ajili ya teknolojia na kwamba DIT inahusika zaidi kutoa mafunzo.

Aidha, Dk Nyari alisema mfumo huo wa kuunganisha gesi asilia badala ya mafuta ya petroli unasaidia kupunguza gharama kwa wamiliki wa magari na kiasi kidogo cha gesi asilia kinatumika katika umbali mrefu.

“Mfumo huu una faida nyingi ambapo gesi asilia yenye ujazo wa kilo moja ni Sh 1,450 huku petroli lita moja ikigharimu zaidi ya Sh 2,200, ukiweka gesi asilia unaweza kwenda umbali mrefu zaidi ambapo kilo moja ya gesi asilia inaenda zaidi ya kilometa 20 huku petroli lita moja inakwenda kilometa 12. Mtungi wa gesi asilia wa kilo 15 unaweza kutumika kutembea kilometa 200 tofauti na petroli,”alisema.

Akifafanua, Dk Nyari alisema miongoni mwa magari 150 yaliyounganishwa na mfumo huo wa gesi asilia, ni ya biashara ya Taxify na Ubber kwa Jiji la Dar es Salaam. Alisema ili mteja aweze kubadilishiwa mfumo wa gari yake kutoka petroli hadi kutumia gesi asilia inamgharimu Sh milioni 1.8 kwa gari lenye ukubwa wa cylinder nne na zaidi ya hapo bei inapanda kidogo.

“Tunachokifanya ni kuwa hatuondoi mfumo wa gari uliopo, bali tunaongeza mfumo mwingine ambapo kutakuwa na mfumo wa petroli na gesi, hii inatoa fursa kwa mmiliki wa gari kuweza kutumia petroli ukiishiwa unarudi kwenye gesi.” Kuhusu uchaguzi wa mazingira Nyari alisema: “Gesi yetu hii ni safi haichafui mazingira.

Hivyo huu ni wakati wa kuachana na matumizi ya petroli na kuhamia kwenye matumizi ya gesi asilia ambayo ni yetu.” Aliongeza kuwa: “Tumefika hapa ili kuzungumza na wabunge ili kwa nafasi yao waweze kuishauri serikali kuongeza wigo huo ili kukuza uchumi na kufikia uchumi wa viwanda.

Pia tunaiomba serikali ipanue wigo wa mtandao wa gesi,”alisema. Akizungumzia changamoto iliyopo, Dk Nyari alisema ni uwepo wa kituo kimoja cha kujazia gesi asilia kwenye magari ambacho kiko eneo la Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam.

“Sisi kama DIT tumejipanga kutafuta mbia ili aweze kuweka kituo kingine pale DIT na kadri wateja watakavyopatikana tutaweka sehemu mbalimbali, kuelekea barabara za Nyerere, Kilwa, na Tegeta.”
Akizungumzia mikakati ya DIT, Dk Nyari alisema wanatarajia kufanya majaribio kwa magari yanayotumia mafuta ya dizeli ambapo kwa sasa wako kwenye mazungumzo na Wakala wa Mabasi ya Haraka (UDART) na ili wafanye majaribio.

Hivi karibuni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) liliambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu kutekeleza mradi wa CNG Dar es Salaam ambao unatarajia kugharimu Sh bilioni 5.7. Shirika hilo lilisema pia kuwa wanafanya mazungumzo na DART ili mabasi zaidi ya 300 ya mwendokasi ambayo yanatarajiwa kuingizwa nchini yatumie gesi asili ili kupunguza gharama za mafuta kwa wastani wa asilimia 40.

Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum, Felister Bura (CCM) alipongeza jitihada za taasisi hiyo na kusema kuwa hatua hiyo itasaidia kujenga uchumi wa nchi. Naye, Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay (CCM) alionesha kufurahishwa na mfumo huo na kudai kuwa utasaidia wananchi kuondokana na gharama za mafuta ya petroli kwenye magari.
 
Madhara ya hyo system kwenye gari..
1. Perfomance ya gari inashuka 10% or more
2. Life span ya engine inapungua
3. Storage ya gari inapungua kutokana na hyo mitungi
4. Gari huwa zinasumbua kwenye kustart au kujerk kwenye ikiwa idle
5. Ajali ya moto iwapo comnection hazikufanyika vizuri
 
View attachment 1119962

Sasa kwa vurugu la hiyo mitungi tyre spare inatoleka kweli?
 
Madhara ya hyo system kwenye gari..
1. Perfomance ya gari inashuka 10% or more
2. Life span ya engine inapungua
3. Storage ya gari inapungua kutokana na hyo mitungi
4. Gari huwa zinasumbua kwenye kustart au kujerk kwenye ikiwa idle
5. Ajali ya moto iwapo comnection hazikufanyika vizuri

mhn! kwa hali hii ushanitoa kwenye soko faster
 
Hiyo milion 1.8 ya kuunganisha mfumo huu ni Bora nifanyie service gari Yangu itakuwa kama mpya.
Hiyo mitungi na jua letu hili la kibongo kila siku mabomu yatalipuka barabaran
 
Back
Top Bottom