Abuu Kauthar
JF-Expert Member
- Jul 10, 2011
- 4,296
- 6,492
Gas gan yauzwa kilo 1500 wakati mtungi wa kilo 15 ni elf 50?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
1.8m..??? Maedeleo hayana vyamaView attachment 1119962
TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeanza kuunganisha magari kwenye mfumo wa matumizi ya gesi asilia badala ya petroli na kwamba hadi sasa magari 150 yamekwishaunganishwa.
Akizungumza katika viwanja vya Bunge, Mratibu wa Mradi wa Matumizi ya Gesi Asilia kwenye magari (CNG Vehicle Project) kutoka DIT, Dk Esebi Nyari alisema pamoja na idadi hiyo ya magari 150 wanatoa mafunzo zaidi kwa wataalamu kuhusu mfumo huo. Alisema katika kutekeleza mradi huo wanashirikiana na kampuni ya wazawa ya Energo Tanzania Limited ambayo ni kwa ajili ya teknolojia na kwamba DIT inahusika zaidi kutoa mafunzo.
Aidha, Dk Nyari alisema mfumo huo wa kuunganisha gesi asilia badala ya mafuta ya petroli unasaidia kupunguza gharama kwa wamiliki wa magari na kiasi kidogo cha gesi asilia kinatumika katika umbali mrefu.
“Mfumo huu una faida nyingi ambapo gesi asilia yenye ujazo wa kilo moja ni Sh 1,450 huku petroli lita moja ikigharimu zaidi ya Sh 2,200, ukiweka gesi asilia unaweza kwenda umbali mrefu zaidi ambapo kilo moja ya gesi asilia inaenda zaidi ya kilometa 20 huku petroli lita moja inakwenda kilometa 12. Mtungi wa gesi asilia wa kilo 15 unaweza kutumika kutembea kilometa 200 tofauti na petroli,”alisema.
Akifafanua, Dk Nyari alisema miongoni mwa magari 150 yaliyounganishwa na mfumo huo wa gesi asilia, ni ya biashara ya Taxify na Ubber kwa Jiji la Dar es Salaam. Alisema ili mteja aweze kubadilishiwa mfumo wa gari yake kutoka petroli hadi kutumia gesi asilia inamgharimu Sh milioni 1.8 kwa gari lenye ukubwa wa cylinder nne na zaidi ya hapo bei inapanda kidogo.
“Tunachokifanya ni kuwa hatuondoi mfumo wa gari uliopo, bali tunaongeza mfumo mwingine ambapo kutakuwa na mfumo wa petroli na gesi, hii inatoa fursa kwa mmiliki wa gari kuweza kutumia petroli ukiishiwa unarudi kwenye gesi.” Kuhusu uchaguzi wa mazingira Nyari alisema: “Gesi yetu hii ni safi haichafui mazingira.
Hivyo huu ni wakati wa kuachana na matumizi ya petroli na kuhamia kwenye matumizi ya gesi asilia ambayo ni yetu.” Aliongeza kuwa: “Tumefika hapa ili kuzungumza na wabunge ili kwa nafasi yao waweze kuishauri serikali kuongeza wigo huo ili kukuza uchumi na kufikia uchumi wa viwanda.
Pia tunaiomba serikali ipanue wigo wa mtandao wa gesi,”alisema. Akizungumzia changamoto iliyopo, Dk Nyari alisema ni uwepo wa kituo kimoja cha kujazia gesi asilia kwenye magari ambacho kiko eneo la Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam.
“Sisi kama DIT tumejipanga kutafuta mbia ili aweze kuweka kituo kingine pale DIT na kadri wateja watakavyopatikana tutaweka sehemu mbalimbali, kuelekea barabara za Nyerere, Kilwa, na Tegeta.”
Akizungumzia mikakati ya DIT, Dk Nyari alisema wanatarajia kufanya majaribio kwa magari yanayotumia mafuta ya dizeli ambapo kwa sasa wako kwenye mazungumzo na Wakala wa Mabasi ya Haraka (UDART) na ili wafanye majaribio.
Hivi karibuni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) liliambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu kutekeleza mradi wa CNG Dar es Salaam ambao unatarajia kugharimu Sh bilioni 5.7. Shirika hilo lilisema pia kuwa wanafanya mazungumzo na DART ili mabasi zaidi ya 300 ya mwendokasi ambayo yanatarajiwa kuingizwa nchini yatumie gesi asili ili kupunguza gharama za mafuta kwa wastani wa asilimia 40.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum, Felister Bura (CCM) alipongeza jitihada za taasisi hiyo na kusema kuwa hatua hiyo itasaidia kujenga uchumi wa nchi. Naye, Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay (CCM) alionesha kufurahishwa na mfumo huo na kudai kuwa utasaidia wananchi kuondokana na gharama za mafuta ya petroli kwenye magari.
Sasa kama wenyewe wanasema kilo moja ya gesi inatembea zaidi ya kilomita 20 inakuwaje tena wanasema mtungi wa kilo 15 unawezesha kutembea kilomita 200? Hawaoni kuwa wanajichanganya katika maelezo yao wenyewe? Maana mimi nilitegemea wangesema huo mtungi utawezesha kutembea zaidi ya kilomita 300 badala ya hizo 200.View attachment 1119962

Huo ni wastani, maana kuna foleni na parameters nyingineSasa kama wenyewe wanasema kilo moja ya gesi inatembea zaidi ya kilomita 20 inakuwaje tena wanasema mtungi wa kilo 15 unawezesha kutembea kilomita 200? Hawaoni kuwa wanajichanganya katika maelezo yao wenyewe? Maana mimi nilitegemea wangesema huo mtungi utawezesha kutembea zaidi ya kilomita 300 badala ya hizo 200.
[emoji3][emoji3][emoji3]Naona dangote ameanza kujaribu kutumia gas magari yanayobeba cement
Hahahah tena hio ni Bullimistic Missiles,😂😂😂Wataalamu wa gesi msaada hapo.
Hiyo hesi hailipuki kama hii tunayopikia au ni ileile? Maana isije ikawa mtu unatembea na bomu kwenye gari.
unaweza kusema russia ananyelea ukraine[emoji3][emoji3][emoji3]View attachment 1682441
Ha ha haukishaweka hyo mitungi buti halitatumika tena
Infact haipaswi kuitwa conversion Bali addition (ya mitungi ya gesi).Yaani wameshindwa ku convert tank ya mafuta na kuifanya ikawa ya gas wameona waeke mitungu kwenye space ya mzigio?
Mafundi wa bongo pasua kichwaYaani wameshindwa ku convert tank ya mafuta na kuifanya ikawa ya gas wameona waeke mitungu kwenye space ya mzigio?
Mafundi wa Kenya unawalinganisha na wanaofunga gesi hapo DiT?Overview:
Mfumo mzuri na nafuu kwenye umiliki wa gari, maana gari si kununua tu bali gharama inakuja kulihudumia hasa upande wa mafuta kwa nchi kama zetu.
Kuhusu mlipuko sio kitu cha kuhofia endapo mahesabu ya kitaalam yatahusishwa hasa umakini wakati wa kuifunga, ndio maana tank ya petrol ilopokaa na ilivyounganishwa kwenda kwenye engine bay utagundua kuna mahesabu yametumika na sio kubuni tu. Jirani zetu Kenya wanaitumia hasa 'matatu' zao na hadi leo sijasikia janga na ilihali kwao ajali ni nyingi zaidi.
Kiufundi nimeokoteza moja, spark plug zinashauriwa ziwe CNG ili ziweze kumudu walau mwaka mmoja. LPG ni baridi sana kufananisha na gas ya mafuta ya petrol. Hii itasaidia huo ugonjwa uliosemwa na mdau kuhusu 'car idling' .