Ditopile: Nchi yetu inaaminiwa ndiyo maana inakopesheka

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
843
Reaction score
1,024
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amewataka wanasiasa nchini kuacha kubeza na kupotosha jitihada zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kukopa huku wakijua fika kwamba ili Nchi ikopesheke ni lazima iwe imekidhi vigezo vya kiuchumi vya kupatiwa mikopo hiyo.

Ditopile ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kitendo cha Tanzania kukopesheka kimeonesha jinsi gani Nchi yetu inaaminiwa.

" Nchi haikopesheki tu hovyo kuna mambo ya kiuchumi lazima yazingatiwe, jambo la kwanza inaangaliwa na kupitiwa taarifa ya ustahimilivu wa deni kwa miaka 10 iliyopita na baada ya kuridhika na ustahimilivu huo pili inaangaliwa matarajio ya miaka 20 ijayo. Mchakato huo unaangaza uwiano wa pato la mwaka na uuzaji wa bidhaa zetu nje pamoja na pato la mwaka na deni la Taifa ambapo ili ufuzu viwango vya kukopesheka Tanzania inapaswa uwiano huo usizidi asilimia 55.

Kwa takwimu za Benki ya Dunia na IMF, zinaonesha uwiano wetu Tanzania upo chini ya asilimia 30 ambayo ni hali nzuri sana na itachukua zaidi ya vizazi viwili kufikia hiyo asilimia 55 na zaidi ya vizazi vinne kufikia asilimia 75 ambacho ndio kiwango hatari cha ukopeshaji," Amesema Ditopile.

Mbunge Dtopile ameongeza kuwa," " IMF na Benki ya Dunia zimeipongeza Nchi yetu kwamba pamoja na mlipuko wa Uviko-19 na vita ya Urusi na Ukraine uchumi wetu umekua mstahimilivu na haujatetereka hata kidogo. Na kwamba hali yetu ya deni na kukopesheka ipo vizuri. Niwasihi Watanzania wenzangu tuendelee kumuombea na kumuunga mkono Rais wetu.

Mbunge Ditopile amewataka watanzania kuwapuuza wanasiasa ambao wanafanya upotoshaji kuhusu mikopo ambayo Serikali inakopa na kwamba mikopo hiyo inakopwa kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa watanzania.

" Rais wetu Dkt Samia hajikopei kwa mambo yake binafsi anakopa kwa lengo zuri la kuleta maendeleo kwa watanzania, na kukopesheka ni sifa nzuri kwa kuwa unaaminika na ni mlipaji mzuri.

"Wapo pia baadhi ya wanaobeza safari za Rais nje Nchi lakini niwaambie kupitia safari hizo uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje umeongezeka, uwekezaji wa ndani, uwekezaji wa pamoja kati ya wazawa na wageni umeongezeka mara nne ndani ya miezi mitano iliyopita. Miradi 132 yenye thamani ya Sh Trilioni 7, 50 (FDI), 30 uwekezaji wa ndani na 52 ya wazawa na wageni.

Chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Nchi yetu imerudishwa kwenye mpango wa fedha za MCC ambapo ziara yake nchini Marekani Novemba mwaka huu imezaa matunda na sasa tumerudishwa kwenye mpango huo ambao wote tunakumbuka miaka ya nyuma ulituwezesha kwenye miradi ya REA na Barabara ya Dodoma-Kondoa-Babati hadi Minjigu," Amesema Ditopile.

Ameongeza kuwa ziara ya royal tour iliyofanywa na Rais Dkt Samia imezaa matunda mazuri kwani vivutio vyetu vya Utalii vimeweza kung'aa duniani ambapo Zanzibar na Arusha vimekua ndani ya vivutio 21 bora duniani.

" Februari mwaka huu Rais Dkt Samia wakati wa ziara ya falme za kiarabu kwenye maonesho ya biashara ya Dubai ameshuhudia utiaji wa saini ya hati ya makubaliano za miradi 36 ambayo Ina thamani ya Sh Trilioni 17.8.

Miradi hiyo imelenga kutoa ajira 204,575 hadi kufikia mwaka 2026, hizi ni jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wetu katika kurejesha mahusiano ya kidiplomasia kupitia diplomasia ya uchumi, kuvutia wawekezaji wa nje kuipa nguvu sekta ya utalii bila kusahau uuzaji na usafirishaji wa bidhaa zetu nje," Amesema Ditopile.

Amewataka watanzania kuendelea kufanya kazi na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwani ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake ametekeleza mambo makubwa katika kila sekta ikiwemo Elimu, Afya na Maji.

IMG-20221230-WA0223(2).jpg
 
Attachments

  • IMG-20221230-WA0222(2).jpg
    IMG-20221230-WA0222(2).jpg
    64 KB · Views: 18
  • IMG-20221230-WA0221(2).jpg
    IMG-20221230-WA0221(2).jpg
    61.3 KB · Views: 19
Kukopa siyo sifa hata kidogo.

Kukopa siyo jambo la kujivunia.

Ni mjinga tu ndiye atayefurahia kukopa kopa.

Badala ya kubuni mbinu na njia za kuongeza mapato ya serikali kupitia ukusanyaji wa kodi ulio bora na kubana matumizi yasiyo na tija, wao wanajivunia kukopeshwa!

Akili gani hii? Akili ya wapi hii?

Play stupid games, win stupid prizes.

Ipo siku yatatutokea puani….
 
naona tunaendelea kushabikia ujinga kwa maslahi binafsi ya kisiasa..

Mbunge baada ya kufikiri na kuishauri serikali namna bora ya kuongeza mapato na Taifa kujitegemea, anashadadia Taifa kukopa.
 
Mbunge wa hivi ndio anategemewa kulisaidia Taifa hili masikini na changa kupiga hatua.
 
Kukopa siyo sifa hata kidogo.

Kukopa siyo jambo la kujivunia.

Ni mjinga tu ndiye atayefurahia kukopa kopa.

Badala ya kubuni mbinu na njia za kuongeza mapato ya serikali kupitia ukusanyaji wa kodi ulio bora na kubana matumizi yasiyo na tija, wao wanajivunia kukopeshwa!

Akili gani hii? Akili ya wapi hii?

Play stupid games, win stupid prizes.

Ipo siku yatatutokea puani….
Serikali hupata mapato kupitia Kodi,tozo,faini..unaposema ibuni njia mpya za mapato unamaanisha ibuni njia mpya za kumkamua mtanzania yuleyule inayemkamua kwa njia zingine za zamani,ili upate vyanzo vipya au kuongeza makusanyo ni kuleta wawekezaji,pawe na investments ambazo zitachachua shughuli nyingine za uchumi,uchumi hauendi bila miundombinu,Sasa tunazo trillions za kujenga bwawa,sgr,barabara nk!?..kopa,miradi ikianza kuingiza utalipa
 
Sidhani kama anazo za kumtosha.. Mikopo, madeni ni utumwa
Barabara zote za lami ni mikopo isipokua barabara ya nzega-tabora,tusingekopa kujenga lami tubaki na barabara za dar-mwabza,dar-mtwara kisa kukopa utumwa!?..masikini ndiyo hudhani kukopa vibaya,mo dewji ana madeni kuliko mtanzania yoyote
 
naona tunaendelea kushabikia ujinga kwa maslahi binafsi ya kisiasa..

Mbunge baada ya kufikiri na kuishauri serikali namna bora ya kuongeza mapato na Taifa kujitegemea, anashadadia Taifa kukopa.
Huwezi ongeza mapato bila kuyafanya raia wako wazalishe,huwezi kuyafanya raia wazalishe bila kuwekeza,huwezi kuwekeza Kama huna fedha,huwezi Songa kiuchumi Kama huna miundombinu ya kusaidia shughuli za kiuchumi,ndipo kukopa ili ujenge miundombinu na kuvutia wawekezaji kinapokuja
 
Ana uelewa mkubwa wa uchumi na fedha kuliko wewe,wewe ni mbumbumbu kwenye uchumi,fedha na kuendesha serikali

Mawazo haya ndio uelewa mkubwa wa uchumi na fedha na kuendesha serikali?

Jaribu kufikiri vizuri.
 
Serikali hupata mapato kupitia Kodi,tozo,faini..unaposema ibuni njia mpya za mapato unamaanisha ibuni njia mpya za kumkamua mtanzania yuleyule inayemkamua kwa njia zingine za zamani,ili upate vyanzo vipya au kuongeza makusanyo ni kuleta wawekezaji,pawe na investments ambazo zitachachua shughuli nyingine za uchumi,uchumi hauendi bila miundombinu,Sasa tunazo trillions za kujenga bwawa,sgr,barabara nk!?..kopa,miradi ikianza kuingiza utalipa
Nimesema mbinu na njia zilizo bora [kuliko zilivyo sasa hivi] sambamba na ubanaji wa matumizi.

Hukuelewa nilichokiandika/ ulichokisoma?
 
Laana tu zinamnyemelea.

Unafurahia kua na uongozi wa kukopaa, unakopa tuuu unakopa !!
 
Mawazo haya ndio uelewa mkubwa wa uchumi na fedha na kuendesha serikali?

Jaribu kufikiri vizuri.
Nchi inahitaji miundo mbinu,tunatoa wapi trillions za kujenga miundombinu!?..hebu jaribu kuishauri serikali pa kupata hizo fedha za miradi
 
NN umenena.

Sijui nicheke??? Anayodai huyo Binti?? au Nilie!

Ulimbukeni nao ni sifa.
(eniwei, wanajuana kwa vilemba).

Ilani ya CCM ndio itatupeleka kule kwa waAsia wanaofurukuta. Ndio kutatupeleka waliko Wagiriki, Ndio kutatupeleka waliko waLebanizi.
Yaani wameshasahau ripoti ya Pandora!!!!
Ndio maana Nchi za magharibi hazileti umang'aa kwa Falme ya Kiarabu....Madeni

Anatuambia Mikopo ambayo ni Madeni.

...tupige kura kwa uangalifu mkubwa. Tukatae ilani ya CCM.
 
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amewataka wanasiasa nchini kuacha kubeza na kupotosha jitihada zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kukopa huku wakijua fika kwamba ili Nchi ikopesheke ni lazima iwe imekidhi vigezo vya kiuchumi vya kupatiwa mikopo hiyo.

Ditopile ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kitendo cha Tanzania kukopesheka kimeonesha jinsi gani Nchi yetu inaaminiwa.

" Nchi haikopesheki tu hovyo kuna mambo ya kiuchumi lazima yazingatiwe, jambo la kwanza inaangaliwa na kupitiwa taarifa ya ustahimilivu wa deni kwa miaka 10 iliyopita na baada ya kuridhika na ustahimilivu huo pili inaangaliwa matarajio ya miaka 20 ijayo. Mchakato huo unaangaza uwiano wa pato la mwaka na uuzaji wa bidhaa zetu nje pamoja na pato la mwaka na deni la Taifa ambapo ili ufuzu viwango vya kukopesheka Tanzania inapaswa uwiano huo usizidi asilimia 55.

Kwa takwimu za Benki ya Dunia na IMF, zinaonesha uwiano wetu Tanzania upo chini ya asilimia 30 ambayo ni hali nzuri sana na itachukua zaidi ya vizazi viwili kufikia hiyo asilimia 55 na zaidi ya vizazi vinne kufikia asilimia 75 ambacho ndio kiwango hatari cha ukopeshaji," Amesema Ditopile.

Mbunge Dtopile ameongeza kuwa," " IMF na Benki ya Dunia zimeipongeza Nchi yetu kwamba pamoja na mlipuko wa Uviko-19 na vita ya Urusi na Ukraine uchumi wetu umekua mstahimilivu na haujatetereka hata kidogo. Na kwamba hali yetu ya deni na kukopesheka ipo vizuri. Niwasihi Watanzania wenzangu tuendelee kumuombea na kumuunga mkono Rais wetu.

Mbunge Ditopile amewataka watanzania kuwapuuza wanasiasa ambao wanafanya upotoshaji kuhusu mikopo ambayo Serikali inakopa na kwamba mikopo hiyo inakopwa kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa watanzania.

" Rais wetu Dkt Samia hajikopei kwa mambo yake binafsi anakopa kwa lengo zuri la kuleta maendeleo kwa watanzania, na kukopesheka ni sifa nzuri kwa kuwa unaaminika na ni mlipaji mzuri.

"Wapo pia baadhi ya wanaobeza safari za Rais nje Nchi lakini niwaambie kupitia safari hizo uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje umeongezeka, uwekezaji wa ndani, uwekezaji wa pamoja kati ya wazawa na wageni umeongezeka mara nne ndani ya miezi mitano iliyopita. Miradi 132 yenye thamani ya Sh Trilioni 7, 50 (FDI), 30 uwekezaji wa ndani na 52 ya wazawa na wageni.

Chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Nchi yetu imerudishwa kwenye mpango wa fedha za MCC ambapo ziara yake nchini Marekani Novemba mwaka huu imezaa matunda na sasa tumerudishwa kwenye mpango huo ambao wote tunakumbuka miaka ya nyuma ulituwezesha kwenye miradi ya REA na Barabara ya Dodoma-Kondoa-Babati hadi Minjigu," Amesema Ditopile.

Ameongeza kuwa ziara ya royal tour iliyofanywa na Rais Dkt Samia imezaa matunda mazuri kwani vivutio vyetu vya Utalii vimeweza kung'aa duniani ambapo Zanzibar na Arusha vimekua ndani ya vivutio 21 bora duniani.

" Februari mwaka huu Rais Dkt Samia wakati wa ziara ya falme za kiarabu kwenye maonesho ya biashara ya Dubai ameshuhudia utiaji wa saini ya hati ya makubaliano za miradi 36 ambayo Ina thamani ya Sh Trilioni 17.8.

Miradi hiyo imelenga kutoa ajira 204,575 hadi kufikia mwaka 2026, hizi ni jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wetu katika kurejesha mahusiano ya kidiplomasia kupitia diplomasia ya uchumi, kuvutia wawekezaji wa nje kuipa nguvu sekta ya utalii bila kusahau uuzaji na usafirishaji wa bidhaa zetu nje," Amesema Ditopile.

Amewataka watanzania kuendelea kufanya kazi na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwani ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake ametekeleza mambo makubwa katika kila sekta ikiwemo Elimu, Afya na Maji.

View attachment 2463353
Yani huo ukoo wa ditopile ni ukoo wa ovyo sana familia nzima ya mzuzuli ni kama ina laana mimi nawajua vizuri .... kwa muundo wa ccm ulivyo ni lazima chama kitajaa mazuzu wengi sana .
 
Back
Top Bottom