Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanapenda sana mi b00 hawa kutwa kuhangaika na abdala kipara
Diva anapendaga kujifanya cute mwenyew, yan anatumia nguv nying kuonekan baby face wakat lizee kabisa
JAMBO limezua jambo
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amemvaa prizenta wa Kipindi cha Ala za Roho cha Redio Clouds FM, Lovennes Malinzi Diva kwa madai kwamba amemtangaza mitandaoni kuwa amepachikwa ujauzito na mume wa mtu ambaye ni densa wa Nasibu Abdul Diamond , Moses Peter Moze Iyobo , jambo ambalo ni uongo.
Prizenta wa Kipindi cha Ala za Roho cha Redio Clouds FM, Lovennes Malinzi Diva Akizungumza kwa masikitiko ya hali ya juu, Aunt alisema kuwa hakutegemea mtu kama Diva angetumia nafasi yake ya utangazaji kumchafua akimsingizia kuwa ni mjamzito, jambo ambalo limemsababishia matatizo kwenye ndoa yake na mumewe Sunday Demonte.
Mwanamke kuwa mjamzito si jambo baya lakini kunichafua mbele ya jamii eti nina mimba ya Moze Iyobo, imeniuma sana. Hebu vuta picha wakwe , mawifi na mashemeji ambao tayari wameshasikia na kusoma kwenye ukurasa wa Diva, akisema mimi nina mimba ya yule mtoto, dah ! Nimeumia sana, kwa kweli siwezi kuliacha lipite hivihivi.
Staa wa sinema za Kibongo , Aunt Ezekiel Grayson Huyo Diva lazima nitasimama naye mahakamani, alisema Aunt. Hivi karibuni , kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diva aliandika: Wakati sakata la mtoto mzuri Aunt Ezekiel ana mimba ya Moze Iyobo likipamba moto, mimba ambayo ni tangu Mwezi wa Ramadhan, sasa hesabuni miezi , hapa ni miezi miwili au mitatu.