Diva, B12, na Mchomvu wapigwa chini Clouds

deonova

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
742
Reaction score
419
DIVA, B 12, MCHOMVU ‘OUT' CLOUDS
by GLOBAL

Stori:- MUSA MATEJA

WATANGAZAJI maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi ‘B 12', Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva', wamepigwa chini na kituo hicho, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa nidhamu wa watangazaji hao.

Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.

Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo alikiri.

"Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.

"Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu," alisema Ruge bila kufafanua zaidi.

Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: "Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana."

Source: GPL
DIVA, B 12, MCHOMVU ‘OUT' CLOUDS – Global Publishers

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Sidhan kama kuna tatizo,maana kazi yao ni kuuza maneno,so wataenda uza kwingine,halafu watangazaj huwa na tabia za kuponda redio nyingine wanapokua redio flan,sijui huwa wanawaza kuwa sehemu 4 life,wakaombe kazi mwananchi communication,
 
Yamekuwa hayo? Hao ndio ntoleee tena sidhani kama watarudishwa,ndio maana Joseph kusaga anaachana nao ameenda kuweka makazi Abu dhabi na kuanzisha redio nyingine huku kushaaribika,Wasiwasi kashasepa Daaaa Clouds inakufa kama majembe yameondolewa kwishneyyyyyy!
 
Moja ya kosa ni baadhi yao kuhudhulia show ya vinega.
 
watangazaji wa kituo kimoja redio kimewasimamisha watangazsji wake wawili kwa kosa la kumshambulia mbunge wa kigoma kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe kwenye mitandao ya twitter,facebook.. ikumbukwe mbunge huyu imekuwa ni kosa kumwandika kwa kwa mtazamo hasi..

"Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na kampuni" ~ Ruge
 
Moja ya kosa ni baadhi yao kuhudhulia show ya vinega.

Clouds noma sana nakumbuka J2 iliyopita hata Dr. Isaack aliogopa kutaja neno kinega mpaka kwanza akaomba ruhusa kwa ruge kulitaja hilo neno maana mtu teja aliyekuwa anamuhoji aka yake ni kinega,na akasema huyu jamaa jina lake flan aka yake ntakuja kukutajia baadae ndio akampigia simu ruge jamaa anaitwa kinega vp tulitaje hewani? Ruge akamwambia haina noma we litaje.
 
wana mgonjwa wa kili pale anaitwa Kibonde... sielewi kuku kama yule anaendeleaje kuwepo kazini wakati ameiweka clouds pabaya sana

hata anayopost kwenye facebook yana warrant kufukuzwa kazi kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…