Diva, B12, na Mchomvu wapigwa chini Clouds

Hivi kupigwa chini ndo kusimamishwa?,hawa kweli wa global publ,pole yao.
 
washapiga sana hela za shows za fiesta,na wana mawe ya kutosha sana,ila cha msingi nu kuomba radhi kwani kukosana na mwajiri wako sio mpango tena bila ya kuwa na sababu za msingi
 
Duh! tutasikia mengi. hii yote ni harakati za CHADEMA kuichukia CLOUDS Media
 
Hivi kupigwa chini ndo kusimamishwa?,hawa kweli wa global publ,pole yao.

Msikilize ruge vizuri amesema

“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa
watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo
lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna
ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza
watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,”


Hio ndio imetoka hao ndio bye bye upe upe panchoo b-hitz bila umakini haiwezi kuwa simple nawakilisha arusha kama b-i-g b-r-o-o-k-l-y-n.
 
uzi kama huu upo humu,na wamesema sababu ya wao kufukuzwa ni kukosa kushiriki mwembe yanga,eeeeh haya.
Ila kufukuzwa kasi si ajabu,

Waende wakaungane na Kepteein... sijui yupo radio gani ziku hizi...
 
tutasikia mengi mwaka huu,cdm ni nouma ,vibaraka wa misukule na mapandikizi watajiju!
 
Hiyo ni Clouds FM, redio ya ccm in kind................ Mkuu tungewekewa na mashambulizi ya akina diva hapa dah!
 
bahati yangu hicho kiredio huwa sisikilizagi!!!!

hata kikifa, hakuna athari, zaidi sana kimeharibu watoto wetu
 
Kule kwetu clouds huwa haishiki.. ila huyo Mchovu kama ni Adamu namjua.
 
Kisheria mwajiri akikusimamisha kazi lazima akupe termination letter yenye sababu ya kusimamishwa,kama wamesimamisha kwa mda usiojulikana that means wataendelea kupewa mshahara coz hawajasimamisha pasee,Diva,Mchovu na B12 nendeni mahakamani kama mnaona ni unfair termination,Je mlipewa warning? Kama hamjapewa basi termination haijatenda haki nendeni kwa wanasheria muishataki clouds mlipwe mipunga yenu! Karibuni mtaani muonane na vinega!
 
wafungue clouds fm 'B', na mambo yataenda safi tu, mbona wana vipaji kuliko RUGE?
 
kuna ukweli zaidi ya huu? MACHADEMA acheni majungu
[h=1]DIVA, B 12, MCHOMVU ‘OUT' CLOUDS[/h]

Stori: MUSA MATEJA
WATANGAZAJI maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi ‘B 12', Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva', wamepigwa chini na kituo hicho, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Hamis Mandi ‘B 12'.
Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa nidhamu wa watangazaji hao.
Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo alikiri.
Adam Mchomvu.
"Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.

"Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu," alisema Ruge bila kufafanua zaidi.
Loveness Malinzi ‘Diva'.
Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: "Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana."
 

Mkuu najua we ushamaliza mambo ya skonga, ila apo kwenye kichwa cha sredi umeandika 3 lakini ndani umetaja 2.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…