Diva: Kama huna milioni 500 huwezi kunioa

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Mtangazaji wa Clouds Fm Loveness Malinzi maarufu kama Diva the bawse amefunguka kuwa hawezi akaolewa na mwanaume yoyote bila kutokew mahari ya shilingi milioni 500.

Hii sio mara ya kwanza kwa Diva kuweka kigezo cha kuolewa na mwanaume mwenye pesa mbele kwani mara nyingi amekuwa akisema kuwa hawezi akaolewa kwa mahari ndogo.

Siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Diva amekumbushia Tena vigezo vikubwa kwa mwanaume ambaye atakubali amuoe ambavyo ni awe tajiri kiasi ya kwamba aweze kutoa mahari ya milioni 500 lakini pia awe anajua kuongea kingereza:

"Kunioa ni milioni 500….set that jokes aside am deadly serious….make sure uwe unaongea English yenyewe hasa… uwe smart uwe handsome…..uwe loaded…No broke niggas in 2018 tupendane kwa faida, you can say wheteves just heard worse, seen worse SMHFG Nothing mean to me…..harsh ain’t new to me I heard it all…..Mwenye povu hana hela ruksa na povu lako nina Omo na jiki plus toothbrush na Colgate jus there for you dummy”.

Diva ametangaza ruksa mwenye hizo sifa ajitokeze hii imekuja baada ya kuachana na mpenzi wake msanii wa Bongo fleva Heri Muziki baada ya kutoswa hewani.


Mpekuzi
 
Naona anachoringia yy mbona wenziwe wanacho au yake ya dhahabu
 
Aliyemtoa usichana ukute alimtoa bure,na aliyempa connection ya kupata kazi Clouds ukute alimla bure,kwanini muoaji aje aoe kwa hela yote hiyo?

Ukute ana mapungufu kibao ikiwa ni pamoja nakutoa kaharufu kwenye nanii kama ilivyosemekana kwa Wolper,wadada hawa,aya bhana kila la kheri.
 
As long as atakuwa haendi chooni kama wanawake wengine au binadamu wengine basi tutatoa hiyo pesa....
 
Maisha yanamchanganya, Kashatumika sana huyo kikongwe nani aje atoe hiyo millioni 500 kirahisi rahisi, Hatudanganyiki.
 
Yete mwenyewe Diva hajawai kuwa na mill 500. Atajioa mwenyewe hakuna mtz wa kumlipia izo pesa
 
Hiyo ni dalili ya kutokuwa na uhakika wa ndoa,wanawake huanza kwa maringo na dharau kubwa kwa vijana hku akijichagulia wa kum... miaka ikisogea wanaanza kuokoka ili wapate waume miaka ikisogea zaidi wanazlishwa na kubakia wakilalamika ovyo '" ooh mi siwezi kuolewa nlishakataa kabisa ndoa mateso...wanaume wenyewe hawaeleweki"" kumbe hana jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…