DIVA, MCHOMVU&B-DOZEN hawajatimuliwa CLOUDS FM

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Na laani mtindo huu watu wanao fahamika fahamika hapa bongo kubuni vitu ambavyo wakati mwingine ni vya kijinga kwa lengo la kujiongezea umaarufu.

Uvumi ya kwamba clouds fm imewatimua vijana maarufu kwa utangazaji yaani b-dozen, adam mchomvu pamoja na diva ni taarifa za uongo na za kupuuzwa kama zilivyo taarifa nyingine za kipuuzi.

Kwa watu ambao wamekuwa wafuatiliaji wa sekta hii ya burudani mtakubaliana namimi kuwa si mara ya kwanza kwa Mchomvu kuandikwa kwenye magazeti kuwa amefukuzwa Clouds wakati katika hali halisi alikuwepo Arusha sababu ya likizo ya kikazi.

Nani asiyejua kuwa huu ni mwezi dume kibiashara? nani asiyejua kuwa hao vijana wapo likizo ya kikazi? Ruge una ubavu wa kuondoa hayo majembe matatu kwa mara moja? Halafu mbadala wao ni kina nani? Perfect? Phillip Mwihava? hahahahaahaha

Clouds fm acheni kuchezea akili za watu, umaarufu hautengenezwi kwa skendo zisizo na maana, hao vijana hawajafukuzwa ila wapo likizo. Umma umedanganywa ili wananchi wawe na hamu yakuja kuwasikiliza pindi vijana hao watakapo rejea.

UPDATE...
Hatimate Adam Mchomvu na Dozen wanashaanza kutangaza Cloud fm, ile siku mi nimesema kwamba ule ulikuwa ni mchezo watu walitokwa sana na mapovu.... asahivi popote pale walipo najua sura zimewashuka
SLIM SHADE
 
Ni kweli walisimamishwa labda wameona ni big loss kuwapoteza wot kwa pamoja wameona bora yaishe
 
kwa hiyo yale maneno aliyokuwa amenukuliwa ruge yalikuwa ni ya uongo.?? au na ww unatafuta kick???
 
We unatuchanganyia habari tu. Una ushahidi gani? Weka hadharani tujue au wewe ndo unatafuta umaarufu.
 
We kwani HR wa clouds mpk uwemkaaaali kuwa hawakufukuzwa au kusimamishwa?we tetea hoja kwa ushahidi si blah blah tu hayo maneno ya utetezi hata kwenye khanga yapo.Kama kweli watarudi hiyo kwamba ni big loss kuwatimua hiyo yako chelsii walimtimua special one ndio hiyo hao 3 clouds?
 
Nimeona diva na baba jonii wame post wakionyesha wamerudishwa kazin maana Jana walikuwa wanapost post za kutafuta sympathy kwa mashabiki wao. .diva nae Leo kapost kwa nyodo kuwa hawez kuwaacha mashabiki wake obviously wamerud kazin now
 
Hivi divaa aliishia na Prezoo,na Zito
Maana akambwaga Zitto kisaa Prezooo
 
B12 WA CLOUDS FM AZUNGUMZIA ISHU
YAKE YA KUSIMAMISHWA KAZI

Hamis Mandi aka B12 mkali wa pindi la XXL ni
miongoni kati ya watangazaji wa Clouds walio
subirishwa kazi ya utangazaji kutokana na madai
ya chinichini ya kuwa wamekiuka sheria na
taratibu za Clouds Media inavyotakiwa
kuendeshwa.

±

Baada ya chanzo chetu kuzinasa taarifa hizo,
kiliamua kumvutia wire B12 live bila chenga naye
akamwagika kimtindo huu,
“Mimi bado nipo Clouds media sema tu
sipo kwenye kipindi now lakini mwezi wa
pili nitakuwa ndani ya kipindi ukitaka full
details zungumza na uongozi wa Clouds
Media hope utafahamu zaidi things follow
apart” – B12.


Source:lindiyetu-Fahari ya kusini

FAHARI YA KUSINI MWA TANZANIA: B12 WA CLOUDS FM AZUNGUMZIA ISHU YAKE YA KUSIMAMISHWA KAZI
 
Mtoa mada anaweza akawa sahihi kiasi fulani na wakati pekee ndio huongea.

Inawezekana kabisa clouds media group wakawa wana cheza na akili za watu hili ku create attention kwenye redio yao au kipindi cha xxl.

Clouds media grouop wanajua fika hata watu wasio penda kuwasikia watataka kuwasikiliza hili kujua hatma ya hao watangazaji.

Clouds media group wanajua fika kuna watu wangependa kusikia hao watangazaji wamefukuzwa.

Sasa walicho fanya clouds media inawezekana wamewapa likizo hadi february huku wakiacha wametengeneza scandal hili wajulikane wamefukuzwa kitu ambacho sicho.

Na ukifatilia mazingira ya hii issue utagundua hii imetengenezwa mahususi kwa manufaa yao.
 
inawezekana kuna ukweli kuwa wanatafuta umaarufu.
 
Time will tell...hata mimi naungana na wewe kuomba Mungu iwe kama unavyotamani iwe kwani katika mazingira ya kawaida tu nikifungua xxl nikamkosa b12 huwa napata sababu tosha ya kuhama stesheni.

Kama ni kweli kuna utovu wa nidhamu umetokea na kiongozi wao hawakuwa tayari kuuweka utovu huo hadharani....labda ni serious ishu...na hata mimi na wewe sidhani kama tutamvumilia mtu anayekuharibia ndani ili hali picha yake nje ni nzuri na anasifiwa kila kona.

Ukimfumania mkeo na houseboy wako ndani kwako, utamchekea kwa kuwa tu majirani wote wanakusifia kuwa wewe ndiye mwenye mke bomba mtaa mzima ?

All in all....Twangala anaweza kurekebika kama ni kweli amekosea....namuaminia sana huyu mchizi....Ila clouds kuja kuunda tena timu kama hii...sio kazi rahisi...na yeyote atakayewachukua amelamba dume.

Popote watakapopokelewa hii timu basi kuna uwezekano mkubwa wakaenda na mashabiki wao...clouds wawe tayari kwa ushindani mzito kwenye hili.

....Au huu ujio wa Azam unahusika....labda jamaa wameahidiwa donge nono...wakaambiwa waharibu ili watolewe nduki.....kesho na keshokutwa tutawasikia wapo Azam Tv........Fetty naye mbona hasikiki.....ni shidaa.....

.....Wakimchukua tena na Millard........uuuuwiii...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…