Bob Mkandara,
Just think of this case and this scenario.
Uko kwenu Ukerewe, ni mkulima na una kaduka kako. Mbunge wenu Msekwa au Mongella, anarudi nyumbani baada y akukumbwa na sekeseke ya tuhuma za uhujumu, kufuja mali na hata ufisadi (wizi).
Mwenyekiti wa Kijiji na yule wa tawi la CCM pale kijijini, wakiandamana na katibu tarafa wanakuja pitisha harambee ya kutaka kondoo, kuku, mbuzi, ngombe, mchele, mkungu wa ndizi ili kuandamana kwenda Nansio kumpokea Mbunge wenu Msekwa/Mongella kwa kurejea nyumbani baada ya kujiuzulu kwa tuhuma.
Wewe si CCM, ni independent au tuseme ni Chadema, CUF au DP. Unakataa kutoa "mchango" huu wa sherehe. Tuseme kukataa kwako hakuhusiana hata chembe kuwa wewe si Mwana CCM au ni hukumu yako juu ya Mbunge wako, bali ni utashi kuwa hutaki changia.
Wanakukalisha kikao na kuanza kukuchimba mkwara na vitisho;
- ohh, Mukandara unajitenga?
- unajiona wewe ni bora?
- huogopi Polisi ambao ni CCM? na Rais wa nchi ni CCM?
- hivi ukifiwa nani atakusaidia kuzika?
- mahindi yako yakikomaa nani atakusaidia kuvuna?
- unafikiri kiduka chako tunakitegemea sana?
- umesahau kuwa Serikali ni ya CCM? na CCM ndio iliyotupa Tanzania Uhuru?
- je watoto wako shule anayokwenda ni nani kajenga kama si CCM?
- kama si CCM wewe ungepata wapi huu utajiri wako mbuzi?
- sisi tutakutenga na si mwenzetu!
- mazao yako siku ukiyaleta gulioni tutahakikisha umedoda
- endelea kuringia vimbuzi na vikuku vyako, wewe ni nani kuigomea CCM!
Halafu taratibu, wenzi kijijini wanaanza kujitenga nawe, watoto wanalishwa sumu shuleni na kuanza hata kukushangaa kwa msimamo wako huku shuleni wameimba CCM kupitia TANU ilituletea uhuru kutoka mkoloni. Leo Baba inakuaje unakataa kuisaidia CCM?
Kumbe Bob Mkandara yule mbuzi na kuku ni mbegu ya kuzalisha mbuzi na kuku wengine ili mwanao Msafiri anayemaliza darasa la saba apate karo ya kwenda sekondari!
This is what I am talking about Divided perspectives. Si ajabu wengi walioandamana waliburuzwa kwa vitisho, wakapewa Khanga, Kofia na chupa moja ya Wanzuki.
Lakini ni mpaka lini tutaendelea na hii disconnection?