Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,362
- 1,133
I repeat and I will repeat...problem is with the Media!
Thomas Jefferson once said that informed citizenry is the only true repository of the public will.
Mwanahabari,
Umeipata wapi hii mkuu, imenivutia sana...
Small nations are like indecently dressed women. They tempt the evil-minded. - JK Nyerere
Mimi katika suala hili nitatoa maono yangu.
Siku moja katika pita zangu nilikuwa ktk mji wa Bukoba bahati nzuri siku hiyo ndipo ilikuwa kesi ya Lwakatare inahukumiwa. Nilichokiona pale ndio maana baadhi ya watu wakisema tuna demokrasia kwanza mimi nakataa na nitakataa milele. Tanzania ni nchi yangu lakini demokrasia tulionayo imeambatana na woga ambavyo vinasababishwa na vitisho kutoka kwa viongozi either wa serikali au chama tawala.
Katika kuanzisha mfumo wa vyama vingi mwalimu aliona hili. hata mtanzania alipopewa uhuru aseme tu kama anataka vyama vingi au kimoja. Wengi walifikiria kwamba mawazo yao yatachukuliwa na watakuwa ktk matatizo wakasema chama kimoja. Ni busara tu za mwalimu tuna vyama vingi.
katika suala lililoko tanzania huko nyuma hapa hapa niliwahi kusema tumalizane huku huku tukitegemea kubadilisha uongozi kwa kutumia masanduku ya kura tumeliwa.
Haya yanayoonekana monduli na bariadi ndiyo hali halisi. hao watu wakati mwingine hawana hata chakula.
Mafisadi wanapeta na kutudhiaki na kutunyoshea mikono kuonekana kama hatuna hoja na hatuwezi kuwanyima usingizi. haya yote nayasema na narudia kuyasema katiba ya nchi yetu ni nzuri lakini haina experience.
Hawa MAFISADI inatakiwa wawe wamezuiwa na sheria mama. Mtu yeyote akipatikama amefanya UFISADI hana haja hata ya kutoka pale alipo. Taifa letu linaangamia kwa sababu ya sheria za 47.
Hapa ni kulazimisha tubadili katiba ya nchi hili MAFISADI wakamatwe mara moja na kufukuzwa katika ofisi na kuondolewa kinga. Hili halitakuja kirahisi tuhakikishe linawezekana.
Mkuu wangu Rev.
Hapo ndipo suala zima la civic education linapokua la muhimu,no wonder ccm hawataki kabisa kusikia kitu kama hicho coz badala ya kupokelewa kama shujaa,basi CHENE angerushiwa mikuki yaani ile ya kibaka style!
Tanzania tunachekesha sana,ukiiba kidogo utapigwa mawe,ukiiba kikubwa basi wewe utaonekana hero.Damn!
Sasa bado mramba,sidhani kama kule Rombo wanamuona hero bado
Kuna kijana aliitikia mwito wa kurudi baada ya kukutana na JK mare 2 US jamaa kaamua kupangua na kurudi Dar .Alikuja na mambo mengi sana juu ku invest.Jamaa majuzi nimekutana naye anakunywa cvhai anashangaa aliyo ambiwa kwamba yameboreshwa serikali ni ngumu na amejaribu kumpa JK akashindwa nikampa simu ya JK direct , JK akasema nenda mahala fulani utasaidiwa hadi sasa ni hadithi baada ya miezi 5 kaamua kurudi US na anasema anaweza asiipende TZ kaama wasemayo Viongozi si mambo ni mchezo kwa maisha ya watafuta maisha .
Kuna kijana aliitikia mwito wa kurudi baada ya kukutana na JK mare 2 US jamaa kaamua kupangua na kurudi Dar .Alikuja na mambo mengi sana juu ku invest.Jamaa majuzi nimekutana naye anakunywa cvhai anashangaa aliyo ambiwa kwamba yameboreshwa serikali ni ngumu na amejaribu kumpa JK akashindwa nikampa simu ya JK direct , JK akasema nenda mahala fulani utasaidiwa hadi sasa ni hadithi baada ya miezi 5 kaamua kurudi US na anasema anaweza asiipende TZ kaama wasemayo Viongozi si mambo ni mchezo kwa maisha ya watafuta maisha .
Hivi katika kumbu kumbu zenu ni lini ilikuwa mara ya mwisho ambayo Chenge alifanya mikutano mikubwa namna ile kwenye jimbo lake akiwa anahimiza maendeleo kabla kukutwa na wimbi la wizi wa pesa mikataba ?Hizi ni pesa za IPTL na it is time I call upon PCCB kua act na si kusema SFO wanachunguza .Bahati mbaya ni kwamba PCCB nayo ni chafu so haiwezi kitu kwa Chenge .
Nilikuwa Arusha Siku Lowasa Akitarajia Kuwa Kule Bbada Ya Kutimuliwa Uwaziri Mkuu, Madereva Walipewa Lita 15 Za Petroli, Huko Bariad Nako Si Haba, Ukweli Unabaki Kuwa Inabidi Wananchi Wakombolewe Kiuchumi Halafu Kifikra, La Sivyo 2010 Ccm Ikiweka Jiwe Kama Mgombea Linaweza Kupita ! Umaskini Wa Kijijini Unawafurahisha Sana Mafisadi, Walioko Bariadi Wanasema Siku Chen Ge Alipojiuzulu Bariad Nzima Iliririma Kwa Vifijo, Polepole Ikaundwa Kamati Ya Mmapokezi Huenda Imetumia Zaidi Ya Tshs 200m, Kutengeneza Mchezo Huu Wa Kuigiza, Tunajifariji Kitu Kimoja Wananchi Hawashangilii Mafisadi Toka Moyoni, Wanashangilia Tu Kwa Njaa Na Mambo Yatabadilika Baadaye, Inshallah Mungu Atalitetea Taifa Lake, Na Ccm Itavunjika Kama Dola La Kiruni
Pamoja na kuunganishwa kwa mada mbili ambazo zinaonekana kufanana lakini zenye mwelekeo tofauti, naomba niendelee na hoja ya Divided Perspective.
Nafikiri inabidi tuke chini na kujiuliza how do we re-connect hawa ndugu zetu ambao wameendelea kuona CCM ni bora na hata kuandamana na kuishangilia pale inapoonekana dhahiri kuwa CCM haifanyi mambo kwa manufaa ya Taifa?
How can we reach these souls that have been intimidated by CCM authority and declare to them that they are independent to do as they please as long as they don't break the laws?