Divock Origi: Nampenda zaidi Ali Kiba

geometry

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2014
Posts
466
Reaction score
358
Hivi karibuni kiungo wa kimataifa wa Kenya anayekipiga katika klabu ya Southampton Victor Wanyama alimtaja mwanamuziki wa kizazi Alikiba kwamba ndio muimbaji anyemkubali zaidi kutoka nchini Tanzania

Kenya imeendelea kuwa moja ya eneo lenye soko kubwa kwa wasanii wa Bongo Fleva – na hii imeendelea kudhihirika baada ya mshambuliaji wa Liverpool, raia wa Belgium mwenye asili ya Kenya Divock Origi ameungana na Wanyama kwa kusema hakuna msanii wa muziki ndani ya mipaka ya Afrika Mashariki anayemkubali kama muimbaji wa wimbo ‘Lupela’ Alikiba.

“Unajua mama yangu huwa ana CDs za muziki kutoka Kenya sana, napenda ngoma za Alikiba sana kuliko Diamond ama hao wengine,”alisema Origi, akiongea nyumbani kwake huko Merseyside, United Kingdom na mwandishi wa Pulse Kenya.
 

Huu ujjinga mnaopost kila kukicha ndio unaompotosha kiba kila siku..wakati diomond anakesha studio na wasanii wakubwa na ku shoot video na makampuni makubwa kila kukicha..yeye kiba kwa mwaka kanyimbo kamoja halafu video yenyewe imejaa tembo fisi na twiga ...mshamdumaza hata kufikiria vizuri hawezi tena
 
Washabiki wa msanii aliefundishwa kiingereza na wema wanatokwa povu,kila siku nasema hapa ni kosa kumpambanisha diamond na king kiba,kiba ni habari nyingine,mpambanisheni diamond na baba kaila
 
Aliulizwa kuhusu wasanii wawili(Simba na kiba) au alitajiwa na wengne???
 
Hakuna tatizo yeye akisema anamkubali kiba ( wapo wengi tu wanasema wanamkubali kiba ) ndio maana wataalamu wa muziki wakaleta vipimo vya nani anapaswa kutambuliwa kama yuko juu ya mwenzake na si bla bla ( na ndio maana Michael Jackson " R.I.P"anatambulika kama mfalme wa POP hadi leo hii kwa vigezo na masharti si maoni ya fulani sio kwamba aliongea Kobe Bryant ) VIPIMO VINATUAMBIA DIAMOND YUKO JUU YA WASANII WOTE WATZ SI BLAH BLAH,ILA NAMBA NDIO SHAHIDI TOSHA.
 
Kiba ni sawa na Timbulo,kumfananisha na Diamond ni matusi makubwa sana
 
Endeleeni kumdanganya tu huyo kiba.Ila mwisho wa siku atakuja kuwalaumu.
 
The Good Thing About Music is When it hits you, you feel no pain...

Team Tunapenda Mziki Mzuri.
 
Hivi hawa wote p square kofiolomide mafikizolo iyanya na wengineo wanaomsifia diamond hawajui muziki? Tunataka olig na mwenzake wamsifie sammata kafunga goli leo maana naamini ndicho wanachokijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…