Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Madiwani wa jiji la Arusha wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ikimpendeza muda utakapofika achukue fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini ambalo kwa sasa lipo chini ya Mrisho Mashaka Gambo.
Wakizungumza Naibu Meya wa jiji la Arusha, Abraham Mollel na Diwani wa kata ya Themi, Petro Lobora katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichoketi Februari 24, 2025 kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 katika jiji la Arusha wamemuomba Makonda achukue fomu kwa kigezo kwamba wanamuamini.Hata hivyo Makonda hakujibu chochote kuhusiana na kauli hizo.