Diwani kuwadhalilisha watumishi Manispaa ya Moshi ni jambo lisilokubalika

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Agosti 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa Manispaa ya moshi kikao cha Baraza la madiwani kiligeuka kama kamati kwa ajili ya kujadili masuala ya kiutumishi hivyo sisi ambao hatukuwa wajumbe kanuni zilituondoa ndani ya ukumbi .

Kikao kiliendelea kwa muda na hatimaye kikamalizika na sisi tukaitwa . Baadae alisimama mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi ,Mwajuma Nasombe ambaye alimkaribisha mstahiki Meya Zuberi Abdallah Kidumo kutoa taarifa ya maamuzi yaliyofikiwa kwenye kamati ya maadili .

Mstahiki Meya alianza kutoa taarifa ya watumishi saba waliokuwa kwenye uchunguzi ambako watumishi wanne kamati iliridhia wafukuzwe kazi kwa utoro wa kutokuwepo kazini kwa muda wa miezi 12. Watumishi wawili kamati iliridhia wakatwe mshahara kwa aslimia 15 kwa kipindi Cha miaka mitatu kutokana na utoro ,hawa walikuwa wanaingia kazini mara moja moja na kuondoka.

Mtumishi mmoja alionekana Hana hatia na kuamuliwa arejeshwe kazini lakini awe kwenye uangalizi kuona mwenendo wake .

Sasa hatua ya pili ikafuata na hii ni taarifa ilyomhusu Diwani wa Kata ya mji Mpya rafiki yangu Abuu Shayo .
Hapa Kila aliyekuwepo ukumbini alikuwa kwenye hali ya utulivu akisikiliza kwa makini Taarifa ikisomwa.
Akisoma taarifa hiyo na maamuzi ya kamati Meya alisema mheshimiwa Diwani alipatikana na hatia ya kuwadhaliisha watumishi wa Manispaa ikiwamo kiwapiga na kuwatolea lugha chafu za matusi .

Tuhuma nyingine ni kuwazuia watumishi hao wasitekeleze majukumu yao kwenye vituo vyao vya kazi .
Kwa wale waliouwepo ukumbini Kila mmoja alionekana akitafakari Taarifa hiyo na kujiuliza maswali mengi hasa ikizingatiwa ya kwamba aliyetuhumiwa kutenda vitendo hivyo ni Diwani mkomgwe ndani ya Baraza la madiwani la Manispaa ya Moshi kwa zaidi ya vipindi vinne.

Niungane na mkurugenzi wa manispaa ya Moshi,Mwajuma Nasombe kukemea kwa nguvu zote kitendo hicho ambacho hakika hakileti taswira nzuri kwa waheshimiwa madiwani . Kitendo cha kuwadhalilisha watumishi wetu ni jambo lisilokubalika na ni kitendo cha hovyo kufanywa na mtu mwenye hadhi ya Diwani .

Ni kitendo Cha hovyo kinachodhalilisha na kutweza utu wa mtu hivyo lazima kikemewe kwa nguvu zote .
Tukumbuke watumishi hawa nao ni binadamu wanastahili kuheshimiwa,kuthaminiwa na si kudhalilshwa.

Pamoja na mstahiki Meya kusema taarifa za Diwani huyo zitasambazwa kwenye maeneo yote ya manispaa ya Moshi ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji ,Diwani Abuu hana budi kutoka hadharani na kuwataka radhi watumishi hawa kutokana na kitendo hicho cha kuwadhalilisha.

Ni rai yangu kwa waheshimiwa madiwani ,heshima mnayopewa na watumishi na watu wengine tukiwamo kina Charles Ndagulla haiwezi kuwa fimbo ama kibali cha kuwafanya muwe juu ya sheria na kufanya haya yaliyofanywa na mheshimiwa Abuu Shayo.

Mwisho na si kwa muhimu ,nikuombe Mstahiki Meya na kamati zenu kutosita kuchukua hatua kwa watumishi na waheshimiwa madiwani wanaokwenda kinyume na miiko na maadili yao na tukio hili liwe funzo kwa madiwani wengine wenye tabia za aina hiyo .

Mwisho kabisa niwape pole sana watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Moshi waliokumbana na kadhia hiyo ,chapeni kazi na mungu atawafuta machozi.

IMG-20260801-WA0093.jpg
IMG-20251204-WA0218.jpg
IMG-20251205-WA0392.jpg

IMG-20251205-WA0384.jpg

IMG-20251205-WA0382.jpg
IMG-20251205-WA0384.jpg
IMG-20251205-WA0384.jpg
IMG-20251205-WA0382.jpg
IMG-20251205-WA0380.jpg
IMG-20251205-WA0367.jpg
IMG-20251205-WA0365.jpg
IMG-20251205-WA0367.jpg
IMG-20251205-WA0365.jpg
IMG-20251205-WA0355.jpg
IMG-20251205-WA0337.jpg
IMG-20251205-WA0337.jpg
IMG-20251205-WA0331.jpg
 
Weka video tuone na kusikiabudhalikishaji
 
Agosti 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa Manispaa ya moshi kikao cha Baraza la madiwani kiligeuka kama kamati kwa ajili ya kujadili masuala ya kiutumishi hivyo sisi ambao hatukuwa wajumbe kanuni zilituondoa ndani ya ukumbi .
Kikao kiliendelea kwa muda na hatimaye kikamalizika na sisi tukaitwa .
Baadae alisimama mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi ,Mwajuma Nasombe ambaye alimkaribisha mstahiki Meya Zuberi Abdallah Kidumo kutoa taarifa ya maamuzi yaliyofikiwa kwenye kamati ya maadili .
Mstahiki Meya alianza kutoa taarifa ya watumishi saba waliokuwa kwenye uchunguzi ambako watumishi wanne kamati iliridhia wafukuzwe kazi kwa utoro wa kutokuwepo kazini kwa muda wa miezi 12.
Watumishi wawili kamati iliridhia wakatwe mshahara kwa aslimia 15 kwa kipindi Cha miaka mitatu kutokana na utoro ,hawa walikuwa wanaingia kazini mara moja moja na kuondoka.

Mtumishi mmoja alionekana Hana hatia na kuamuliwa arejeshwe kazini lakini awe kwenye uangalizi kuona mwenendo wake .

Sasa hatua ya pili ikafuata na hii ni taarifa ilyomhusu Diwani wa Kata ya mji Mpya rafiki yangu Abuu Shayo .
Hapa Kila aliyekuwepo ukumbini alikuwa kwenye hali ya utulivu akisikiliza kwa makini Taarifa ikisomwa.
Akisoma taarifa hiyo na maamuzi ya kamati Meya alisema mheshimiwa Diwani alipatikana na hatia ya kuwadhaliisha watumishi wa Manispaa ikiwamo kiwapiga na kuwatolea lugha chafu za matusi .
Tuhuma nyingine ni kuwazuia watumishi hao wasitekeleze majukumu yao kwenye vituo vyao vya kazi .
Kwa wale waliouwepo ukumbini Kila mmoja alionekana akitafakari Taarifa hiyo na kujiuliza maswali mengi hasa ikizingatiwa ya kwamba aliyetuhumiwa kutenda vitendo hivyo ni Diwani mkomgwe ndani ya Baraza la madiwani la Manispaa ya Moshi kwa zaidi ya vipindi vinne.
Niungane na mkurugenzi wa manispaa ya Moshi,Mwajuma Nasombe kukemea kwa nguvu zote kitendo hicho ambacho hakika hakileti taswira nzuri kwa waheshimiwa madiwani .
Kitendo cha kuwadhalilisha watumishi wetu ni jambo lisilokubalika na ni kitendo cha hovyo kufanywa na mtu mwenye hadhi ya Diwani .
Ni kitendo Cha hovyo kinachodhalilisha na kutweza utu wa mtu hivyo lazima kikemewe kwa nguvu zote .
Tukumbuke watumishi hawa nao ni binadamu wanastahili kuheshimiwa,kuthaminiwa na si kudhalilshwa.
Pamoja na mstahiki Meya kusema taarifa za Diwani huyo zitasambazwa kwenye maeneo yote ya manispaa ya Moshi ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji ,Diwani Abuu hana budi kutoka hadharani na kuwataka radhi watumishi hawa kutokana na kitendo hicho cha kuwadhalilisha.

Ni rai yangu kwa waheshimiwa madiwani ,heshima mnayopewa na watumishi na watu wengine tukiwamo kina Charles Ndagulla haiwezi kuwa fimbo ama kibali cha kuwafanya muwe juu ya sheria na kufanya haya yaliyofanywa na mheshimiwa Abuu Shayo.
Mwisho na si kwa muhimu ,nikuombe Mstahiki Meya na kamati zenu kutosita kuchukua hatua kwa watumishi na waheshimiwa madiwani wanaokwenda kinyume na miiko na maadili yao na tukio hili liwe funzo kwa madiwani wengine wenye tabia za aina hiyo .
Mwisho kabisa niwape pole sana watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Moshi waliokumbana na kadhia hiyo ,chapeni kazi na mungu atawafuta machozi.
Poleni kwa watumishi wote mliodhalilika, lakini pia nanyi hakikisheni hamuwadhalilishi wale wanaokuja kwenu (Halmashauri) kupata huduma.

Karma ipo.
 
Back
Top Bottom