Ndagullachrles
JF-Expert Member
- Jun 20, 2023
- 256
- 259
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Diwani wa Kata Myamba wilaya ya Same, Greyson Kyondo Fue (42), kwa tuhuma za kuendesha gari kwa uzembe na kumgonga mwendesha pikipiki maarufu kama boda boda aliyetajwa kwa jina la Daudi Kibwengo (24), mkazi wa Kijiji cha Myamba na kusababisha kifo chake kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali hiyo.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi kupitia kamanda wake)SACP),Simon Maigwa,tukio hilo limetokea Septemba 4, 2026, katika Kijiji cha Kambeni, Kata ya Myamba, Wilaya ya Same.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Diwani huyo alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.180 DCS, aina ya Mitsubishi Fuso, akitokea Kijiji cha Lugulu kuelekea Mamba Myamba.
Inadaiwa kuwa, akiwa katika uelekeo huo huo na pikipiki yenye namba za usajili MC.710 EXX, iliyokuwa ikiendeshwa na Daudi Kibwengo, mtuhumiwa aliigonga pikipiki hiyo na kusababisha mwendesha pikipiki kujeruhiwa pamoja na uharibifu wa chombo chake.
Baada ya tukio hilo, majeruhi alikimbizwa katika Kituo cha Afya Myamba kwa ajili ya kupatiwa matibabu, hata hivyo alifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari lenye namba za usajili T.180 DCS aina ya Mitsubishi Fuso, kwa kuendesha bila kuchukua tahadhari stahiki kwa watumiaji wengine wa barabara.
Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo sambamba na kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo.
Baada ya kukamilika kwa uchunguzi, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
1.Chini ni picha ya marehemu Kibwengo
2.Picha ya kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro (SACP),Simon Maigwa