Diwani mstaafu apigwa risasi na Askari aliyelewa kwa kutokuvaa Barakoa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Diwani mstaafu wa wadi ya Kiptoror Barnaba Lagat anapokea matibabu katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi Eldoret, Uasin Gishu baada ya afisa wa polisi kumpiga risasi kifuani.

Diwani huyo kwa sasa anapigania uhai wake baada ya kuachwa akivuja damu nyingi baada ya kupigwa risasi kwa kutovalia maski.

Inasemekana kuwa Lagat alipigwa risasi majira ya jioni akiwa katika kituo cha biashara cha Kapsigilai na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Kapcherop.

Daniel Chebet ambaye alishuhudia kisa hicho aliiambia K24 Digital kwamba afisa aliyempiga risasi Lagat alikuwa amelewa na inadaiwa alitumia nguvu nyingi kutekeleza itifaki za wizara ya afya kwenye

Alitoa wito kwa Mamlaka Huru ya Usimamizi wa Polisi (IPOA), kushughulikia swala hilo ili mwathiriwa apate haki.
"Natoa wito kwa IPOA kuingilia swala hili mara moja. Tunataka afisa huyo ashughulikiwe ipasavyo ili kuzuia kutokea kwa visa kama hivyo,” Chebet alisema.

Kufuatia tukio hilo kulikuwa na hali tete katika eneo hilo kwani ilihofiwa kuwa huenda wenyeji wakazusha.
Viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na mbunge Joshua Kutuny walilaani kitendo hicho na kutaka uchunguzi wa haraka kutekelezwa ili mhusika achukuliwe hatua.

Katika ujumbe wake Twitter Kutuny aliwahimiza wenyeji watulie wakati mamlaka zinazohusika zinachukua hatua muhimu kutatua swala hilo.
"Ninataka kuwahakikishia wapiga kura wangu kuwa haki itatendeka, mshukiwa atakamatwa na kushtakiwa ili kutoa mfano kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo," Kutuny alisema.

Hisia za Kutuny ziliungwa mkono na Julius Tunduria mfanyabishara ambaye alisema ukatili wa polisi ni tishio kwa maisha ya binadamu na pia ni ukiukaji wa haki za binadamu.

"Tabia ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi ni jambo la zamani, kwa sasa tuko katika nyakati za huduma ya polisi ambayo inaheshimu maisha ya binadamu na haki za msingi za binadamu," Tunduria alisema.

MCA wa wadi ya Chepsiro / Kiptoror Kipchumba Birir alisema serikali inapaswa kumshurutisha mwathiriwa kugharamia matibabu ya mwathiriwa na pia kumlipa fidia.
 
cc Tony254
 
Kwa ninavyojua in That Banana République of Kunyaland this is not News, just part of Regular Kenya Police practice.
Among police killings niliumia sana juu ya wale vijana wawili wa Embu.
May the Lord rest them Embu brothers in eternal peace.
 
vipi mbowe amefunguliwa kesi ya ugaidi?
 
Kwa ninavyojua in That Banana République of Kunyaland this is not News, just part of Regular Kenya Police practice.
Among police killings niliumia sana juu ya wale vijana wawili wa Embu.
May the Lord rest them Embu brothers in eternal peace.
Kumbe huwa unatazama news za Kenya? Sisi Wakenya huwa hatutazami news zenu.
 
MK254 mnadhahihakiwa. Bora Kenya tungeinunua na kuigeuza kuwa mbuga ya wanyama tu au museum.
Unaongea matope kuhusu nchi yenye uchumi mkubwa kushinda wenu? Banking sector kubwa kushinda yenu? Telecommunication sector kubwa kushinda yenu? Port na airport busy kushinda zenu?
 
Acha kutia aibu. Mmliki wa hivyo ni mkoloni, yaani mkenya wa kawaida hana faida na huo ukubwa maana wazungu huhamishia kwa kila kitu. So hiyo nchi mpaka sasa ilishauzwa. Tuuzine na sisi watz.
 
Sasa hiyo nayo ni sifa?
Sisi tunawajua nje ndani, na sio nyie tu tunaijua Africa na dunia kwa ujumla.
hamna mkenya mwenye akili timamu atakaa chini na aanze kutazama tv za tanzania.....kwanza tv stations zenu hata hatuzijui
 
Juzi polisi Tanzania walipomtia vijiti yule bodaboda Dodoma, hiyo news iliripotiwa na nani hapa JF Kama sio mkenya?
Kuna Wakenya wawili watatu wanaoishi huko kwenu. Pengine hao ndio waliopost. Ila Mkenya anayeishi Kenya hana shughuli na news zenu.
 
Back
Top Bottom