GE2025 Diwani mteule wa ACT na wenzake wengine 10 atuhumiwa na ujambazi

GE2025 Diwani mteule wa ACT na wenzake wengine 10 atuhumiwa na ujambazi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Diwani mteule wa Chama cha ACT Wazalendo, Juma Mzee Shaban, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kigoma pamoja na wenzake kumi, wakikabiliwa na kesi ya ujambazi wa kutumia silaha, kinyume na kifungu cha 287 cha Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16, Marejeo ya 2023).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, imeelezwa kuwa mnamo tarehe 30 Oktoba 2025, katika eneo la Kagera, ndani ya Wilaya na Mkoa wa Kigoma, washtakiwa hao, wakiwa pamoja na wengine ambao bado hawajakamatwa, walitenda kosa la kuwasha moto na kuchoma Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kagera yenye thamani ya shilingi 59,323,800, mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma.

Taarifa zinaeleza kuwa wanachama 117 wa ACT Wazalendo walikamatwa siku ya uchaguzi na siku ya maandamano, akiwemo mgombea ubunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe. Baada ya mahojiano, wanachama 102 waliachiwa huru akiwemo Zitto Kabwe, huku 15 wakibaki rumande.

diwa.png
 
ACT wamefikiwa, hawa ni magaidi na Majambazi, na wahaini, wafungwe! Lisu alishauri achaneni na uchaguzi, limeshinda na Baba level
 
Anaonekana kabisa ni jambazi ..atupwe ndani tu
Hahaha kumbe ukiangalia mtu machoni siku hizi unaweza kujua kama ni jambazi. Sasa kama ni hivyo kwa nini hawakukamtwa mwanzoni hadi wasubirie uchaguzi
 
Waongezee magereza mapya naona wanazidisha hasira Kwa jamii

Raia wanasubiria sababu tu wakinukishe tena
 
Back
Top Bottom