TANZIA Diwani mteule wa CCM Kata ya Shiwinga, amefariki dunia baada ya kunywa maji ya betri

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Aliyekuwa Diwani mteule wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Shiwinga, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Lusekelo Mwalukomo amefariki dunia baada ya kunywa maji ya betri. Tukio hilo lilitokea jana Novemba 26, 2025 na amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mbozi Mission.

Akithibitisha kifo hicho, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega amesema leo Alhamisi Novemba 27, 2025 kuwa sababu za diwani huyo kunywa maji hayo bado hazijajulikana, ingawa taarifa za awali zinahusishwa na msongo wa mawazo.

“Wataalamu wetu wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo halisi. Alikutwa amekunywa maji ya betri saa nne asubuhi. Madaktari walijitahidi kuokoa uhai wake lakini walishindwa,” amesema Mbega.

Mbega amesema anajiandaa kwenda nyumbani kwa familia ya marehemu kwa ajili ya mazungumzo na kupanga taratibu za mazishi kwa kushirikiana na CCM. Kwa sasa, mazishi yanatarajiwa kufanyika Novemba 28, 2025 nyumbani kwake Shiwinga, baada ya kikao cha familia na chama.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augostino Senga amesema hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya tukio hilo iliyofikishwa polisi.

“Sijaipokea taarifa hiyo. Kwa taratibu, tukio kama hilo lazima liripotiwe polisi ili fomu ya matibabu itolewe. Tunaendelea kufuatilia, tukipata taarifa kamili tutatoa maelezo,” amesema Senga.
1764250676047.png
 
Baba mtu mzima kama huyo mpaka anafikia maamuzi ya kukatisha uhai wake anaacha maswali mengi sana.

Sijui kwanini nimeunganisha tukio hili na yaliyotokea Oct 29, labda baba wa watu aliona yasiyosemekana yamemuelemea kashindwa kuhimili…

Anyways, pole kwa familia ya marehemu.
 
Taarifa njema.
 
Wow
163192.jpg
 
Matukio haya yameacha watu wengi tu wakiwa na trauma. Watanzania ambao walikuwa hata hawajui SMG, AK47 na assault rifles zinatoa mlio gani. Watanzania ambao walikuwa hawajaona maiti zilizofumuliwa ubongo na risasi. Watanzania ambao walikuwa wakiona mrundikano wa maiti kama mikungu ya ndizi kwenye vita vya mbali huko Darful, Syria na Congo. Watanzania ambao wameuliwa ndugu zao wakiwa majumbani bila sababu. Watoto wadogo wameona maiti zikiwa zimetapakaa damu huku zimekodoa macho kama kuuaga mwanga...oooh! Kuna trauma kubwa sana. Na hatuna mambo ya trauma counselling wala nini. Ni kila mtu na lwake.

Tutegemee kuwa na watu sugu na wagumu wa hisia na wasiojali cho chote. Na wenye roho nyepesi au watakaozidiwa na msongo wa mawazo ndo hivi wanajiua ili kukwepa mateso yao.

Ni kipindi kigumu sana. Kwa mlio na watoto, kuweni nao karibu. Ongeeni nao. Wasikilizeni na wapeni ushauri. Wakiwauliza maswali kuhusu vifo vile wapeni maelezo mazuri. Wahakikishieni kuwa mnawapenda; na kwamba wao ni wa thamani. Kwamba wako salama na watakua na kutimiza ndoto zao...timizeni wajibu wenu. Kila mtu apambanie kizazi chake kama akina Mwigulu, Samia na Kikwete wanavyopambania vizazi vyao!
 
Aliyekuwa Diwani mteule wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Shiwinga, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Lusekelo Mwalukomo amefariki dunia baada ya kunywa maji ya betri. Tukio hilo lilitokea jana Novemba 26, 2025 na amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mbozi Mission.

Akithibitisha kifo hicho, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega amesema leo Alhamisi Novemba 27, 2025 kuwa sababu za diwani huyo kunywa maji hayo bado hazijajulikana, ingawa taarifa za awali zinahusishwa na msongo wa mawazo.

“Wataalamu wetu wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo halisi. Alikutwa amekunywa maji ya betri saa nne asubuhi. Madaktari walijitahidi kuokoa uhai wake lakini walishindwa,” amesema Mbega.

Mbega amesema anajiandaa kwenda nyumbani kwa familia ya marehemu kwa ajili ya mazungumzo na kupanga taratibu za mazishi kwa kushirikiana na CCM. Kwa sasa, mazishi yanatarajiwa kufanyika Novemba 28, 2025 nyumbani kwake Shiwinga, baada ya kikao cha familia na chama.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augostino Senga amesema hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya tukio hilo iliyofikishwa polisi.

“Sijaipokea taarifa hiyo. Kwa taratibu, tukio kama hilo lazima liripotiwe polisi ili fomu ya matibabu itolewe. Tunaendelea kufuatilia, tukipata taarifa kamili tutatoa maelezo,” amesema Senga.
Wenzie wanakunywa maji toka Marekani....
 
Back
Top Bottom