DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
MGOMBEA Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mwanga Kusini mkoani Kigoma Mussa Maulid amezindua kampeni yake kwa kuwaomba wakazi hao wampigie kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mtindo wa kurundika.
Maulid alisema wakazi hao wakishamrundikia Rais Samia wamrundikie kura nyingi mgombea Ubunge wa Kigoma mjini, Clotus Chipandu Baba Levo sambamba na yeye mgombea udiwani.
Alisema wananchi wakitekeleza hivyo ndio matakwa ya CCM.
"Nawaomba wakazi wa Kigoma ikifika Oktoba tunatiki kwa Rais Samia, tunatiki kwa Baba Levo na tunatiki kwa Mussa Maulid kwa kurundika," alisema Maulid.
Alisema kwamba anawaomba ridhaa wananchi wa Mwanga Kusini kwa sababu ametekeleza maendeleo mbalimbali yakiwemo ujenzi wa barabara wa baadhi ya mitaa kama mtaa wa Simu.
Maulid alisema pamoja na uboreshaji huo wa barabara kwa kiwango cha lami, anajipanga kuendelea na uwekaji wa lami katika mitaa iliyobaki.
Alisema barabara mbili nyingine ziko kwenye mchakato wa kuzoboresha ni Kikamba na Dk Mzazi ambazo atazikamilisha akipata ridhaa ya wananchi atazikamilisha.
Mradi mwingine ulioko kwenye mchakato ni wa ujenzi wa madarasa matatu mapya na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Muungano.
Alisema pia ametekeleza ujenzi wa Ofisi ya Kata kwa gharama ya Shilingi Milioni 64.
Pia kwa kishirikiana na Halmashauri ya Kigoma Ujiji wanatarajia kujenga kituo cha afya, ujenzi wake utagharimu Shilingi 264 zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Aidha, Maulid alisema anatarajia kujenga kituo cha polisi kwenye Kata yake.