Diwani Raibu Juma kutoa dola 5,000 kama utapata video yake akitetea Mapenzi ya Jinsia Moja

Diwani Raibu Juma kutoa dola 5,000 kama utapata video yake akitetea Mapenzi ya Jinsia Moja

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1655510636617.png

Diwani wa Kata ya Bomambuzi Manispaa ya Moshi Raibu Juma akiongea na Redio Moshi Fm kupitia kipindi cha Darasa mseto ameweka wazi kutoa Dollar 5000 ikiwa atapata video inayoeleza kutetea wapenzi wa jinsia moja (Ushoga) katika sherehe aliyohudhuria.

"Ishu ya kuhudhuria sherehe ya wapenzi wa jinsia moja ni uongo ilikuwa sherehe ya kuaga mwaka na kuzaliwa kwa mtu (birthday party) na nilikuta huko viongozi wa Chama na Madiwani,sija wahi kupelekwa kwa kamati ya maadili ilikuwa ni ishu ya kutengenezwa."

"Ninayo video ya Madiwani wakiniomba msamaha nirudi kugombea nafasi ya Umeya baada ya kuona kuwa ninafaa na walidanganywa, Diwani wa Korongoni alikuja kuniomba msamaha na sale".

"Shida ya Madiwani wetu hawasomi,kuna Madiwani ambao siwezi kuwasema hapa kuwa walipewa hela waniondoe katika sakala la Soko la Manyema,ila wafanyabiashara kuondolewa pale ni swala la vikao kisheria."


Credit: Dar Mpya
 
Si ndio huyu mpuuzi aliwaambia wenzake wavue barakoa kwamba hakuna korona Magufuli kaifuta kwa maombi!? Huyu ni mmoja wa Sukuma Gang mwandamizi sanaaa
 
Back
Top Bottom