Diwani wa CCM ateuliwa kuwa mjumbe huku akituhumiwa kwa Mauaji

Diwani wa CCM ateuliwa kuwa mjumbe huku akituhumiwa kwa Mauaji

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2008
Posts
281
Reaction score
66
Diwani anayetuhumiwa kwa mauaji ateuliwa
Source Majira: Monday, 03 August 2009
Na Suleiman Abeid, Kahama

DIWANI wa Kata ya Malunga (CCM) wilayani Kahama mkoani Shinyanga Bw.Jumanne Masomba (67) ambaye kwa sasa yuko mahabusu kwa tuhuma za mauaji, ameteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati za Kudumu ya Halmashauri ya wilaya ya Kahama.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa kamati za kudumu katika Halmashauri ya wilaya ya
Kahama juzi, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Paulo Magazi alimtaja diwani huyo
kuwa ni mmoja wa wajumbe katika Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira.

Kwa mujibu wa majina ya wajumbe wa kamati hiyo yaliyotangazwa na Bw. Magazi, pamoja
na Bw. Masomba wajumbe wengine ni Bw. Daudi Mahona ambaye ndiye Mwenyekiti wa
Kamati, Bw. Alfred Mhanganya, Bw. Hassan Mponya, Bw. Petro Shinzi na Bi. Pili Sonje.

Wajumbe wengine ni Bw. Sostenes Ipagala, Bw. Juma Kimisha, Bw. Telesphory Salia, Bi.
Angela Paulo, Bw. Bundala Kadilana, Bw. Juma Tengesha, Bi. Josephina Balanoga, Bi.
Mary Lundalila, Bw. Joram Gwambasa na Bw. Edward Kalikali.

Bw. Masomba kwa sasa yupo mahabusu katika gereza la wilaya ya Kahama akituhumiwa
kwa kosa la mauaji ya mtumishi mmoja wa hospitali ya Serikali wilayani Kahama marehemu Bernadetor Maziku (40) ambaye alikuwa Katibu Muhtasi wa Mganga Mkuu wa Wilaya.

Tayari diwani huyo ameishafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji ambapo kesi yake imepangwa kutajwa tena katika Mahakama ya Wilaya mjini Kahama Agosti 4, mwaka huu.

Akizungumzia uteuzi wa diwani huyo katika Kamati ya Kudumu huku akiwa mahabusu,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Bi. Theresia Mahongo, alisema
kwa mujibu wa kanuni za madiwani, uwakilishi wa diwani aliyeshitakiwa kwa kosa
lolote la jinai au mauaji utakoma baada ya Mahakama kumtia hatiani kwa kosa
alilokuwa ameshitakiwa na si vinginevyo.

“Ni kweli huyu diwani hivi sasa yupo mahabusu, anakabiliwa na kesi ya mauaji, lakini bado ameteuliwa kuwa mjumbe katika moja ya Kamati za Kudumu za Halmashauri yetu,kanuni za Halmashauri zinaruhusu kwa maana bado Mahakama haijathibitisha kosa lake,” alieleza Bi. Mahongo na kuongeza,

“Madiwani ni tofauti na watumishi wengine kawaida, kwa mujibu wa Sheria za Utumishi
Mtendaji hutakiwa kusimamishwa kazi mara moja pale tu anapokamatwa akituhumiwa kwa
kosa lolote lile la jinai, ni tofauti na viongozi wa ngazi ya kisiasa, hawa uongozi
wao unasita baada ya makosa yao kuthibitishwa na Mahakama,” alifafanua.

Mkurugenzi huyo alitoa mfano wa Mbunge wa Rombo Bw. Basil Mramba ambaye anakabiliwa na mashitaka mahakamani lakini bado anaendelea kuhudhuria vikao vya Bunge kama mwakilishi wa jimbo lake.
 
Nadhani walidhani jamaa kasafiri atarudi ndiyo wakamtangaza ama ndiyo nguvu ya CCM ?
 
Back
Top Bottom