TANZIA Diwani Wa CCM Kata Ya Mzimuni Manispaa Ya Kinondoni Afariki Dunia

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933


Diwani wa CCM Kata ya Mzimuni katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Manufred C. Lyoto amefariki dunia leo Machi 7, 2026

Taarifa za kifo chake zimetolewa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mzimini, Abdalah M. Ally, ambaye pia ametoa pole kwa wanachama wa CCM pamoja na wananchi wote wa Kata ya Mzimini na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kufuatia msiba huo.

Amesema taratibu za mazishi pamoja na taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitatolewa baadaye.

Wakati huo huo, Katibu wa CCM Kata ya Mzimini kwa idhini ya Mwenyekiti, amewaomba wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Kata kuhudhuria kikao cha dharura kitakachofanyika saa 2:30 asubuhi.

#ManaraTvUpdate
 
Kata ya mzimuni. RIP

Next...๐Ÿค”๐Ÿ™„
 
Daaah tukupe nini Baba kwa hizi furaha unazotupa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ