PreGE2025 Diwani wa kata ya Narung'ombe ashiriki kwenye harambee ya kufturisha wanafunzi. Kassim Majaliwa ampongeza

PreGE2025 Diwani wa kata ya Narung'ombe ashiriki kwenye harambee ya kufturisha wanafunzi. Kassim Majaliwa ampongeza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Diwani wa Kata ya Narungombe, Mhe. Khamis Majaliwa, amechangia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Narungombe na Liuguru kwa ajili ya futari katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Harambee hiyo imefanyika Machi 15, 2025, wakati wa mkutano wa Diwani wa Ilani uliowakutanisha wananchi wa kata hiyo. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa

Wananchi na viongozi walioshiriki harambee walichanga zaidi ya shilingi milioni 1.5 ambapo fedha hizo zitatumika kuhakikisha wanafunzi wanapata futari, ikiwemo vyakula na vinywaji, ili kuwasaidia kutimiza swaumu zao kwa utulivu na nguvu zaidi.

Naye Mhe. Kassim Majaliwa amepongeza juhudi za Diwani huyo, akisema ni mfano mzuri wa uongozi unaogusa maisha ya watu moja kwa moja.

diwani hara.png
 
Watanzania wengi sana kwasasa hivi wanashindia mlo mmoja tu kwa siku unaweza kufikiri unafuturisha kumbe ndio unalisha watu Lunch kiingilio ni Salam alekum.

Ni kufeli kwa Sera za Chama chakavu cha CCM kwenye Ajira.
 
Back
Top Bottom