Leo asubuhi nilisikiliza powerbreakfast ya Clouds, Gerald Hando alipanic kweli kweli, kwa jinsi alivyokuwa anafoka yani nadhani mpaka mimate ilimtoka!
Analaumu kwanini watu wameenda kusikiliza wahuni? Kama kuongea ukweli ni uhuni na unaonekana una chuki basi kazi ipo.
Analaumu kwanini viongozi wa CDM wameenda kusikiliza wahuni? Nadhani hajui hii ni nchi huru na kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuunga mkono kile anachoona kina maslahi kwa wananchi.
Anasema watu waliingizwa bure ili wajae. Hahaha. Nina rafiki zangu walifika pale saa 6 usiku (Show iliisha saa 7 usiku) na walilipa kiingilio.
Mi nawashauri clouds wanyamaze tu, maana wanaonekana wanatapatapa.
KUFENI KIMYAKIMYA!