Wakuu kuna ukweli wa taarifa hizi?
- Tunachokijua
- DJ Fetty majina yake kamili ni Fatma Ahmed, amekuwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu. Hivi karibuni kumeibuka taarifa zinazomuhisha kuwa ni miongoni mwa watu waliowekwa pembeni kutokana na kukosa vigezo vilivyowekwa na bodi ya Ithibati (JAB), ingawa yeye mwenyewe bado hajaweka hadharani kuhusiana na jambo hilo.
Madai
Julai 25, 2025 kumekuwa na baadhi ya grafiki zenye utambulisho wa vyanzo tofautitofauti ikiwemo Wasafi, Jambo TV, na Mwanahalisi ikiwa na ujumbe unaokaribia kufanana ukieleza kuwa DJ Fetty amekiri hadharani kwamba yeye amekuwa kada wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa grafiki hizo na kubaini kuwa ni za kughushi.
Taarifa hiyo haijachapishwa na vyanzo hivyo kama inavyoonekana kwenye grafiki hizo na badala ni za kughushi zilizotengenezwa na wapotoshaji kwa malengo yao binafsi.
Hakuna taarifa yoyote kutoka chanzo chochote cha kuaminika kwa hivi karibuni ambayo inathibitisha kuwa Dj Fetty alitamka maneno hayo ama kuhusiana na yeye kuwa kada wa CHADEMA.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Dj Fetty hajachapisha taarifa yoyote kueleza kuwa yeye ni kada wa CHADEMA ama taarifa yoyote kuhusiana na jambo hilo.
Grafiki hizo za kughushi zimetumia aina tofauti ya mwandiko pamoja na mpangilio tofauti ukilinganisha na grafiki halisi zinazotengenezwa na vyanzo hivyo. Tazama Jambo TV, Wasafi na hapa