TANZIA DJ Ommy afariki dunia

TANZIA DJ Ommy afariki dunia

Dah! Mwana sana jamaa ulikua humkosi maisha club ile ya masaki enzi zile kwa wale wazee wa bunyero bunyero.. nadhali alikua pale kama manager... tangulia kamanda
Yes, ndio nimeona pia DJ JD ameelezea. Bunyero bunyero ndio nini mkuu?
 
Wakuu,

Inawezekana wengi mmeshapata taarifa ya kifo cha DJ Ommy lakini kwavile sijaona post hapa JF juu ya hili nimeona nigusie kutokana na umuhimu wake.

DJ Ommy ni moja ya madj wa mwanzo kabisa wa radio ambao walitikisa sana na kuleta mapinduzi hasa ya muziki wa dansi. Wanamuziki wa dansi hasa wa zamani wanajua jinsi alivyowapaisha enzi hizo.

Kipindi cha midundo motomoto pale radio one aliteka nchi kwa mixing zake za bolingo ambazo watu wengi nyakati hizo hawawezi kusahau.

R&B na hip hop namba moja alikuwa John Dilinga akichuana na Bonny Love lakini kwenye yenu pamoja na ukali wa Dj Charles wa Africa bambataa lakini DJ Ommy alikuwa kiboko na aliteka mitaa yote kwa kipindi chake hasa midundo motomoto pamoja na Dj show akiwa na Aboubakary Sadik.

Pumzika kwa amani Dj Ommy #mixingmaster

=====
View attachment 1674182
MMOJA wa Dj bora wa redio hapa nchini, Dj Ommy amefariki dunia juzi jioni.

Kwa mujibu wa mtangazaji wa redio One, Abdalla Mwaipaya ambaye amewahi kufanya kazi naye Dj Ommy ambaye ni miongoni mwa wazilishi wa Kwa fujo djs alifariki baada ya kuugua kw amuda.

Alisema Dj Ommy alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchanganya muziki hasa wa dansi na alikuwa na kipaji cha ubunifu wa jingle za redio.

“Wakati yupo Radio One ndiye aliyebuni jingle zilizokuwa zinawataja watangazaji wote zikiimbwa na Papii Kocha na marehemu Mao Santiago,” aliandika.


“Kwa wale wanaozikumbuka ni ile inaimbwa wajifanya wanajuaaa kumbe waungua juaaa radio one kiboko yao. Dj Ommy amechukua ameweka waa Abubakari Sadiki shangilia ushindi unakuja.. nk,”.

Alongeza alijua kukaa kwenye kipindi chochote iwe Dj shoo au midundo motomoto kitambulisho chake kikubwa kilikuwa ni kicheko chake kilichoacha alama.

TAARIFA:
Ratiba ya kutoa heshima za mwisho kwa DJ OMMY

Saa Tisa alasiri Mwananyamala Hospitali

Saa kumi jioni mwili utaondoka kuelekea Same kwa mazishi

Poleni ndugu,jamaa na marafiki.
 
Duh nilijua huyu DJ Ommy mdogo

apumzike kwa amani
 
Mwenyezi Mungu awafariji Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu
 
Back
Top Bottom