Majok majok
JF-Expert Member
- Aug 3, 2023
- 783
- 2,057
Kuna vimaneno vimeanza kusambazwa na mbumbumbu kuanza kumfananisha Diarra na kipa wao Ayoubu Lakred!
Anayeweza kuwalinganisha wawili hao kwa sasa kwa maana ni Kama unalinganisha kichuguu na mlima!
Unamlinganisha kipa aliyefanya vizuri kwenye mechi 3 dhidi ya kipa aliyeonyesha ubora wake miaka 2 mtawalia!
Ukienda kwenye rekodi bado Ayoubu ni cha mtoto mbele ya Diarra, Diarra kaisaidia timu yake kucheza fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika akiwa na kiwango Bora kabisa na akiwa ni miongoni mwa makipa wa kisasa!
Kachaguliwa na caf kuwa miongoni mwa makipa 10 Bora wa afrika utamlinganishaje na Ayoubu?
Mambo ya kucheza kwa kiwango Cha juu Diarra ni mambo anayoyafanya Kila mechi na imeshakuwa kawaida kwake ndio maana ikitokea akacheza vibaya mechi moja lazima ajadiliwe, habari za kuokoa penalty kwenye hatua muhimu kwake siyo story Tena ishakuwa ni kawaida kwake na ashathibitisha ilo!
Unapataje ujasiri wa kuanza kuwalinganisha hawa wawili? Misimu 2 mfululizo kaisaidia timu yake kubeba ubingwa wa Tanzania akiwa na kiwango Bora uku akiibuka kuwa kipa Bora wa msimu!! unaanzaje kuweka mlinganisho?
Nenda kaangalie timu ya Taifa ya Mali kikosi chote kina wachezaji 2 tu wanaocheza barani Africa na mojawapo ni Diarra kutoka yanga! Waliobaki wote wanakipiga ulaya kwenye timu kubwa kubwa!
Nafikiri kiwango Cha uelewa wa mpira tunatofautiana Kuna wale bendera fuata upepo mashabiki oya oya walioujulia mpira ukubwani, na Kuna wale wazee wa mihemko, pia Kuna wale wanaojua lakini wanajizima data ili wasionekane tu wanampa maua yake kwa kuwa Yuko yanga!
Lakini pia huwezi kumlinganisha mchezaji aliyecheza si zaidi ya mechi kumi na baadhi yake akiwa kafanya vizuri mechi 4 halafu umuweke fungu moja na aliyecheza misimu 2 kwa ubora utakuwa una kichaa Cha mbwa!