Tetesi: Djuma Shabani kutua msimbazi kama mbadala wa Kapombe

Mr Alpha

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
273
Reaction score
765
Simba watamsajili djuma Shabani kama mbadala wa kapombe

Baada ya kuachana na klabu ya Yanga msimu uliopita Na kutua Azam FC, beki wa kulia raia wa Congo DR Djuma Shabani anategemea kujiunga na watani wa jadi Simba SC katika majira haya ya kiangazi.

Djuma ambae amekaa msimu mzima akiwa nje ya uwanja hapo awali alimalizana kila kitu na Azam Fc kabla ya deal hilo kuishia njiani

Simba pia wana haha kutafuta sahihi ya Beki wa kushoto wa YANGA Joyce Lomalisa ambae mkataba wake UNAELEKEA mwishoni

Bangala tayari yupo Azam Fc, Mayele yupo Pyramids Fc , Moloko yupo Libya , Djuma anaenda Simba Sc hao ni baadhi ya wachezaji waliopita Yanga Sc Kwa mafanikio makubwa.
 
Dah kudadeki kama ni hivyo Muhindi tapeli.
 
Hapa ndio sijawahi jua
 
Narudia tena simba wanafanya sajili za kisiasa. yale yale ya kina jobe wakati kwenye ligi tu hawafanyi vizur or hawana record nzuri
 
Kwa uongozi huu usiojua mpira na wachezaji uliopo Simba sasa hivi sio ajabu hizi tetesi za Lomalisa na Juma Shabani zinaweza kuwa kweli. Kama waliwaleta Freddy na Jobe toka nje ya nchi kwa mbwembwe kuwa ni mbadala wa Phiri na Baleke kitu gani tena kitashindikana? Na mbaya zaidi sasa hivi wanasema Freddy ni mali eti ana magoli 14 Zambia na Tanzania ana magoli zaidi ya 10 wakihesabu hata alilowafunga TRA Moshi kwenye FA Cup!!!!

Simba wakifanya mzaha kwenye usajili siwaoni wakitoka kwenye hilo shimo waliloingia. Itawachukua muda mrefu sana kutoka huko na hasa ikizingatiwa Azam anazidi kuimarika kila siku. Mzaha mzaha Simba inaweza kujimilikisha nafasi ya tatu kwa miaka kadhaa ijayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…