Dk. Arnold Kashembe ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Simba SC

Dk. Arnold Kashembe ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Simba SC

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Klabu ya Simba SC imetoa taarifa kuwa imemteua Dr Arnold Kashembe kuwa Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo, isome taarifa ya Simba hapa chini.

Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iiliyokutana jana jioni,kwenye moja ya kumbi za mikutano za Hoteli ya Serena iliyopo hapa jijini Dar es salaam,imemteua *Dr Arnold Kashembe* kuwa katibu Mkuu mpya wa klabu.

Msomi huyo mwenye shahada ya Uzamivu na aliyekuwa Mhadhiri kwenye vyuo mbalimbali barani Ulaya, uteuzi wake unaanza mara moja.

Pia kamati hyo imepanga kufanya Mkutano wake mkuu wa kawaida tarehe 13-8-2017, huku pia ikitarajiwa kufanya Mkutano Mkuu utakaojadili mabadiliko ya katiba tarehe 20-8-2017.


Chanzo:dewji blog

====

Wakati huo huo;

Katibu Mkuu wa Yanga SC, Boniface Mkwasa amemtangaza Dismas Ten kuwa msemaji rasmi wa club hiyo, Dismas anachukua nafasi ya Jerry Muro.

Yanga wamteua Ten kuwa msemaji, Jerry Muro atupiwa virago
 
hizi ni nafasi nyeti lakini sijawahi kusikia hi I nafasi wa simba na yanga wakizitangaza badala yake wanapeana kienyeji
 
Inatia matumaini, muda ndio utatupa majibu halisia
 
Nadhani huyu hatawaambia waandamane

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ana uzoefu wa kudai points FIFA

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom