Dk Bagile: Majadiliano ni msingi wa uponyaji na mustakabali wa Taifa

Dk Bagile: Majadiliano ni msingi wa uponyaji na mustakabali wa Taifa

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
544d6086-61e7-4e8b-976a-0111f19080c7.jpg

Geneva, Uswisi. Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Women in Social Entrepreneurship, Dkt. Astronaut Bagile, ametoa wito kwa Serikali, wadau wa maendeleo, asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla kuimarisha majadiliano ya kitaifa na mshikamano wa kijamii ili kuponya majeraha ya kitaifa na kujenga Tanzania yenye amani, haki na ushirikishwaji.

Dkt. Bagile alitoa wito huo alipozungumza katika tukio maalumu lililofanyika sambamba na Kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) mjini Geneva, Uswisi Machi 11, 2026.

Alisema matukio ya vurugu na mpasuko wa kijamii yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi wa Oktoba 2025 yameacha athari kubwa kwa jamii, hasa kwa wanawake, vijana na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi.

Kutokana na hali hiyo, alisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za makusudi za kujenga upya uaminifu, kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuweka mazingira ya majadiliano jumuishi kwa ajili ya mustakabali wa taifa.

“Nguvu ya Tanzania imo katika utofauti wake. Hata hivyo, nguvu hiyo inaweza kudhihirika kikamilifu pale tunapoungana, tukavua tofauti zetu na kujenga mustakabali wa pamoja unaozingatia amani, haki na mshikamano,” alisema Dkt. Bagile.

Alisisitiza kuwa, majadiliano ni nyenzo muhimu ya uponyaji wa taifa kwa kuwa yanatoa fursa kwa sauti za waliodhuriwa kusikika, changamoto kujadiliwa kwa uwazi na suluhisho za pamoja kupatikana kwa njia ya amani.

Dkt. Bagile pia alitoa rai kwa wadau wote kushiriki kikamilifu katika juhudi za kujenga amani kuanzia ngazi ya jamii hadi taifa kwa ujumla. Alisisitiza umuhimu wa kulinda haki za binadamu, kuimarisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya kijamii na kitaifa, pamoja na kukuza utamaduni wa kusikilizana na kuheshimiana licha ya tofauti zilizopo.

Kwa mujibu wa Dkt. Bagile, Tanzania ina fursa ya kugeuza kipindi hiki kuwa mwanzo wa ukurasa mpya wa matumaini, ustahimilivu na umoja wa kitaifa.

Alisema kwa ushirikiano wa pamoja, Watanzania wanaweza kurejesha uaminifu, kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuweka msingi imara wa taifa lenye ustawi na fursa sawa kwa wote.

Alisisitiza kuwa, wakati Tanzania ikiendelea kuimarisha demokrasia, haki na utulivu wa jamii, ni muhimu kwa wadau wote kuchukua hatua za pamoja sasa ili kujenga taifa lenye amani, maridhiano na maendeleo endelevu.
 
Hakuna mahali popote ambapo Mungu ameelekeza tujadiliane n.a. Shetani
 
Tunaweza vipi kujadiliana wakati kiongozi mkuu wa chama cha upinzani yuko jela tuwe serious kidogo
 
Uwajibikaji na uwajibishwaji kwanza halafu ndo mengine….
 
Back
Top Bottom