Gerad2008
JF-Expert Member
- Jun 9, 2009
- 583
- 287
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni(farao)
siku za mwisho wa kampeni zinavyozidi kwisha ndivyo na wagombea ubunge wasiokubalika kama Dk. Batilda Buriani wanavyozidi kuchanganyikiwa na kujikuta wakitoa ahadi ambazo za kuwatia hasira wapiga kura.
Jana pale Moshoni stendi Batilda aliwaahidi wapiga kura vijana kwamba wakimchagua atawalipia wote kodi za pango na wataishi nyumba za kupanga bure bwerere!!!!.
Jamani jamani huyu mama atatoa wapi hizo hela za kuwalipia vijana zaidi ya laki 5 kama siyo kutaka kutuambia yeye ni fisadi na anataka kutakatisha hela chafu.
Kwa kweli wananchi walilalamika sana kwani hakuna aliyetarajia kama huyu DK siku za mwisho atapoteza hata zile kura chache alizotegemea kupata.
Wazee, vijana na akina mama wameshtuka na WAMEAPA ATAWATAMBUA SIKU YA TAREHE 31/10/2010 kama wao ni Mazezeta au watu na akili zao.