Dk. Biteko awataka Viongozi kuepuka uuzaji wa ardhi, wajikite kutatua migogoro

Dk. Biteko awataka Viongozi kuepuka uuzaji wa ardhi, wajikite kutatua migogoro

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amewataka viongozi nchini kuepuka vitendo vya kuuza ardhi, badala yake wajikite katika kutatua migogoro inayohusiana na ardhi.

Ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Aprili 23, 2025, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Sekondari Migungani, Wilaya ya Monduli, ikiwa ni sehemu ya ziara yake kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Dk Biteko amesema katika maeneo mbalimbali nchini, kuna viongozi wanaojihusisha na uuzaji wa ardhi za vijiji ambazo tayari zina migogoro, au kujimilikisha hiyo ni kinyume cha sheria, akionya watakaobainika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ameongeza kuwa Serikali ina lengo la kuhakikisha wafugaji nchini, wakiwemo wa Wilaya ya Monduli wanaheshimiwa na kuthaminiwa kutokana na mchango mkubwa wa sekta ya mifugo katika uchumi wa Taifa, unaokadiriwa kufikia asilimia saba ya pato la Taifa.

Screenshot 2025-04-23 195919.png
 
Back
Top Bottom