Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Katika taarifa yake kwa umma aliyoitoa hivi karibuni, Dk Malisa amesema, karibu mwaka mmoja baada ya mauaji hayo, familia za waliopoteza maisha bado hazijapata haki, ukweli kuhusu matukio hayo haujawekwa wazi kikamilifu, na waliohusika hawajawajibishwa.
Amesema tangu matukio hayo, asasi za kiraia, viongozi wa dini, familia za waathirika na wananchi wamekuwa wakitoa wito wa kuundwa kwa Kamati Huru ya Kitaifa ya Maridhiano na Ukweli itakayoongozwa na wananchi, lakini juhudi hizo hazijapata mwitikio kutoka kwa Serikali.
Kwa mujibu wa Dk Malisa, kamati hiyo itakuwa na jukumu la kubaini ukweli kuhusu yaliyotokea, kutambua waathirika, kuhakikisha familia zao zinapata fidia na msaada, kupendekeza hatua za uwajibikaji na mageuzi, pamoja na kuweka msingi wa uponyaji na maridhiano ya kitaifa.
Katika hatua hiyo, ameiomba EU, Bunge la Ulaya na nchi wanachama wake kutumia ushirikiano wao wa kidiplomasia na Tanzania kushawishi Serikali kushiriki kwa nia njema katika mchakato huo.
Pia ameitaka EU kutumia mazungumzo ya kisiasa kati yake na Tanzania kuhimiza uwajibikaji, maridhiano na ulinzi wa nafasi ya asasi za kiraia, akipendekeza masuala hayo yazingatiwe katika kuendeleza ushirikiano kati ya pande hizo.
Aidha, ameitaka EU kuunga mkono asasi huru za kiraia, vyombo vya habari na taasisi za kidini zinazofanya kazi ya kuandika na kuhifadhi ushahidi kuhusu matukio hayo na kusaidia waathirika.
Ombi jingine ni kwa EU kushinikiza Serikali kuweka wazi taarifa zote zinazohusu watu waliouawa, waliojeruhiwa, waliopotea na waliokamatwa au kuzuiliwa kiholela kuhusiana na matukio hayo.
Dk Malisa amesema wananchi wako tayari kuunda kamati hiyo wenyewe, akisisitiza kuwa wanachohitaji ni uhakikisho kwamba Serikali haitapuuza tena juhudi za maridhiano.
Ameonya kuwa ukimya wa EU kuhusu suala hilo unaweza kudhoofisha uhusiano wake na wananchi wa Tanzania, akisisitiza kuwa ushirikiano wa kimataifa ni muhimu katika kuhakikisha mchakato wa maridhiano unapata nafasi ya kutekelezwa.
“Hatuitafuti kisasi. Tunatafuta ukweli, haki na nchi ambayo Watanzania hawatauawa tena na Serikali yao,” amesema Dk Malisa katika taarifa hiyo, akihitimisha kwa kauli ya “Kamwe isitokee tena.”
Taarifa hiyo imekuja wakati suala la uchunguzi wa vifo, uwajibikaji na haki kwa waathirika wa matukio ya Oktoba 29, 2025 likiendelea kuwa sehemu ya mjadala kuhusu haki za binadamu na maridhiano ya kitaifa nchini Tanzania.
Dk Malisa ameeleza pia kuwa aliwahi kukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uhaini, na kwamba alikaa gerezani kwa miezi sita.
*****
PRESS RELEASE
DR. GODFREY F. MALISA
P.O.BOX 8283
MOSHI
0752 303463
NATIONAL RECONCILIATION AND TRUTH COMMITTEE (NRTC)
ONE YEAR AFTER THE MASSACRE: TANZANIAN CITIZENS CALL ON THE EUROPEAN UNION TO SUPPORT A PEOPLE-LED RECONCILIATION PROCESS
Dar es Salaam, Tanzania-
Almost one year has passed since Tanzanian citizens were killed by organs of their own government. Families have not received justice, the truth has not been told, and those responsible have not been held accountable.
Since the massacre, civil societies, faith leaders, families of victims, and citizens have repeatedly called for the creation of an independent, people-led National Reconciliation and Truth committee. (NRTC) This committee would be mandated to:
1. Establish the full truth about what happened,
2. Identify victims and ensure reparations and support for their families,
3. Recommend accountability and reforms to guarantee non-repetition,
4. Create a path for national healing.
To date this call has fallen on deaf ears within the Government of the United Republic of Tanzania.
We, concerned Tanzanian citizens, therefore appeal to the European Union, the European Parliament, and EU Member States as long-standing partners of Tanzania and defenders of human rights, democracy and the rule of law:
We ask the European Union to :
1. Publicly call on the Government of Tanzania to accept and participate in good faith in a people-formed Reconciliation Committee;
2. Use its political dialogue under the EU- Tanzania partnership, including the Cotonuo framework, to make reconciliation, accountability and protection of civic space a condition for deeper cooperation;
3. Support independent civil society, media, and faith-based actors working to document the truth and support victims;
4. Urge the release of all information regarding those killed, injured, disappeared, and arbitrarily detained in connection with the events.
The people of Tanzania are ready to form this Committee ourselves. What we need is not permission to reconcile, but a guarantee that the Government will not ignore it again. International pressure, particularly from the European Union, can make participation unavoidable, but if the European Union chose to be quiet we will no longer consider you partners of Tanzanians.
We do not seek revenge. We seek truth, justice, and a country where Tanzanians are never again massacred by their government. We say NEVER AGAIN!
DR GODFREY F. MALISA
COORDINATOR
Nb. I was arrested and charged for Treason. I stayed imprisoned for six months.