Dk. Rose Reuben: Kati ya mauaji 941 yaliyoripotiwa Januari hadi Juni, 2026 mauaji 458 yalitokana na migogoro ya kimahusiano

Dk. Rose Reuben: Kati ya mauaji 941 yaliyoripotiwa Januari hadi Juni, 2026 mauaji 458 yalitokana na migogoro ya kimahusiano

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Watetezi wa haki za binadamu ambao ni wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wametoa wito kwa Serikali na wadau kuchukua hatua ili kukomesha mauaji yanayotokana na migogoro ya mahusiano.

Akizungumza Oktoba 22, 2026 Jijini Dar es Salaam wakati wakisoma tamko la pamoja, Dk. Rose Reuben amesema kwamba mauaji yanayotokana na mahusiano yamekuwa yakiongezeka nchini.

“Kwa mujibu wa takwimu za matukio ya uhalifu za Jeshi la Polisi Tanzania, kwa kipindi cha Januari mpaka Juni 2026, jumla ya matukio 941 ya mauaji yaliripotiwa, ikilinganishwa na matukio 926 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2025. Hili ni ongezeko la makosa 15. Kati ya matukio 941 ya mauaji, 458 sawa na asilimia 42% ni mauaji yanayohusisha migogoro ya kimahusiano.

“Uchambuzi wetu unaonesha kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, mauaji yanayotokana na migogoro ya kimapenzi na mahusiano yamekuwa yakichukua sehemu kubwa ya mauaji yanayoripotiwa na Jeshi la Polisi. Kwa mfano, mwaka 2024 jumla ya matukio ya mauaji yalikuwa 2,193 na kati ya hayo, mauaji 422 yalisababishwa na migogoro ya kimahusiano.”

Wameongeza: “Hali kadhalika kwa mwaka 2025 kuliripotiwa jumla ya matukio 1,977 ya mauaji, na kati ya hayo, matukio 725 ya mauaji yalisababishwa na migogoro ya kimahusiano. Kwa kipindi cha miaka miwili (2024 na 2025) na takwimu za mauaji za nusu mwaka 2026, jumla ya Watanzania 1,605 wamepoteza maisha kutokana na migogoro ya kimahusiano ya kimapenzi. Takwimu zinaonesha kwamba idadi kubwa ya vifo vinavyosababishwa na migogoro ya kimapenzi ni wanawake. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa asilimia 40 ya vifo vya wanawake vinatokana na migogoro ya mahusiano ya kimapenzi.”

Wadau hao wametoa wito kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuanzisha kampeni ya kitaifa ya malezi bora, afya ya akili, uzazi wenye kuwajibika na mahusiano salama.


View: https://youtu.be/8aPUoTD0p1E

Aidha, wametoa wito wa kuhakikisha inaongeza Maafisa Ustawi wa Jamii nchi nzima kwa kuajiri idadi yote ya 18,000 nchi nzima ili kukidhi mahitaji ya jamii katika kushughulikia migogoro na kotoa elimu na unasihi kwa familia zenye migogoro.
 
Back
Top Bottom