Timing mkuu wangu timing ndio muhimu sana.. Hoja za Mafisadi zilikuja mapema sana na sasa hivi umaarufu wa kina Zitto, Dr.Slaa umepwaya inabidi itafutwe mbinu nyingine..Wapiganaji wamesha nunua mada na wananchi wengi hawakumbuki asili ya mzozo huu wa Ufisadi.
Sasa fikiria kama Dr.Slaa angeliangusha kimba la mafisadi wakati huu kungekalika kweli!..Nina hakika Lowassa, Rostam na kundi zima la mafisadi wangefanya madudu mengine kibao ambayo pengine leo hii tungekuwa tumeshawachoka kabisaaa. lakini haraka z3etu zimetufikisha wapi, kimefanyika kitu gani?..NOTHIMG!... sana sana wameachishwa madaraka lakini bado wanaendeleza biashara zao kama kawaida. Wanapewa mikopo na kila baya unalofikiria bado wanafanya kama hakuna uchunguzi wowote ule unaofanyika.
Viwanja vya mijini hasa nyumba za Msajili, Kigamboni na maeneo yote yanayomilikiwa na serikali imekuwa deal kubwa kwa hao hao Mafisadi.. Wao wamesha gawana mapema sasa hivi ni wao wanaoviuza kwa wawekezaji..Ardhi baada ya madini kwisha has become source ya Ufisadi.
Niliyasema haya mwaka juzi kama unakumbuka vizuri! - Ufisadi Kwa kwenda mbele..