1) Kwanza kwa Upemba kule wanasema ni wa "kuchovya" maana ametoka akiwa na miaka minne, ni sawa umwambie Obama akagombee na urais Kenya....au Sepetu akawanie Ubunge kule Sikonge Tabora, au Juma Nhunga atoke Dole akawanie Bariadi alikozaliwa.
2) Dk. Shein toka ahamie Znz kuwa daktari amekuwa yye na hospitali hana social contact, hajihusishi na masual yoyote ya kijamii. Kibaya mtangulizi wake, Marehemu Dk. Omar Ali Juma, alikuwa mtu wa kujichanganya, Shein siye
3) Tokea mwaka 1995, amekuwa mtu wa kubebwa, hana utashi binafsi wa kisiasa, hata hili yeye amekuwa akimuandaa Mohamed Aboud kwa muda mrefu na kwa nia njema kabisa, sasa watu wenye maslahi binafsi wakiongozwa na...... (ntawataja baadaye) ndio wanamsukuma ili watawale Zanzibar
4) Mwaka 1995 Dk. Shein aliiingia katika siasa kwa kuombwa na kina Dk. Salmin baada ya CCM kuwa wanahaha kutafuta watu wa kushindana na CUF Pemba, sasa Shein akaahidiwa hjata akishindwa atapewa Unaibu Waziri na kweli akashindwa akapewa Unaibu wa Afya baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi.
5) Mwaka 1997, Dk Salmin alimuomba tena Shein kuwania ujumbe wa NEC na akamwambia akishindwa atamuomba Mkapa amteue na alipoenda akawa mtu wa pii nyuma ya Mohamed Aboud mkoa wa Kusini Pemba, na alizungukwa kwa kura hii maana yake ni kwamba hana political base.
6) Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2000, Dk. Shein aliomba kazi nje ya nchi na alipata na hiyo ni baada ya kuona kwamba yeye alikuwa kundi la Dk. Salmin na hivyo Karume asingemfaa, lakini Karume akambiwa amchukue na kumuomba tena awanie Mkanyageni, ambako alipata baada ya kushindwa na kura za "Maruhani" za CUF na akateuliwa kuwa Waziri wa Utawala Bora...
Mwaka 2001 kukatokea mauaji Januari, baada ya CUF kupambana na Ngunguri (Mahita, FFU, KMKM, JKU) na kabla hata haijapoa Taifa likapata msiba mzito wa kuondokewa na Makamu wa Rais, Dk. OMar Ali JUma, na Shein akapata tena bahati ya kuteuliwa kuwa makamu wa Rais. Hakugombea wala hakufanya kampeni.
2005 kila mtu anajua hakuwa chaguo la JK na Mkapa na wazee wakamtaka JK amteue kuwa mwenza na kwa mazingira ya wakati ule hakufanya kampeni ila JK alikua na nguvu.