Elections 2010 Dk Slaa awalipua Pinda, Mkapa

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Dk Slaa awalipua Pinda, Mkapa

Salim Said, Singida


MGOMBEA kiti cha urais kupitia Chadema, Dk Willibrod Slaa amemlipua Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisema kuwa akiwa mwenyekiti wa kikao cha kamati ya wabunge wote alimtaka ajitokeze mbele ya wabunge na akanushe kuwa hakutaja kiwango cha mishahara ya wabunge bali magazeti yalimnukuu vibaya.

Dk Slaa amekuwa akieleza kila mara kuwa wabunge wanalipwa mshahara mkubwa tofauti na hali halisi ya uchumi wa nchi na akatamka bayana kuwa watunga sheria hao wanalipwa zaidi ya Sh7 milioni, jambo ambalo alisema ni kufuja fedha za walipa kodi.

Jana kwenye mikutano ya kampeni ya hadhara aliyoifanya katika kata za Igilansoni na Sepuka kwenye Jimbo la Iramba Magharibi jana, Dk Slaa alielezea jinsi msimamo wake ulivyoitingisha serikali na madai kuwa Waziri Pinda alijaribu kumtaka akane kauli yake iliyonukuliwa na vyombo vya habari.

"Nilikataa nikamwambia waziri mkuu kuwa kama mnakataa mshahara wa mbunge si Sh7 milioni, tangazeni kima halisi cha mshahara wa wabunge katika gazeti ili Watanzania wajue," alisema Dk Slaa.

"Lakini waziri mkuu alikataa na kuniomba nisiendelee kulitangaza suala hilo kwa wananchi kwa madai kuwa nawagombanisha wabunge na wapigakura wao.

"Lakini sikumsikiliza kwa kuwa natetea haki ya Watanzania na hivyo niliamua kutoka pamoja na baadhi ya wabunge wenzangu wa Chadema na kupita mikoa mbalimbali kuwatangazia wananchi tofauti hiyo ya mishahara kati ya wabunge na watumishi wa umma."

Dk Slaa aliendelea kusema: "Wakasema watanishitaki nikawambia kama mshahara wao ni siri, wa kwangu sio siri na mimi nilitangaza wa kwangu... kwa kuwa wananchi si wajinga wanajua kuwa kwa kuwa Slaa ni mbunge na Mohammed Misanga ni mbunge, basi kima chao kinalingana."

Dk Slaa alimgeukia rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akimtuhumu kuwa alimtumia mpwa wake, Ole Njolai kwenda kumuhonga ili aache ubunge wa jimbo hilo mara baada ya kuihama CCM 1995. Dk Slaa alikuwa mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema kwa vipindi vitatu.

"Aliniita hotelini Karatu na kuniambia nimetumwa na Rais Mkapa; kama unataka ubalozi, kama unataka kwenda Umoja wa Mataifa (UN) utapata au kama unataka fedha sema ni shilingi ngapi unataka ili uache ubunge na urudi CCM," alisema Dk Slaa.

"Nikamwambia nahitaji mkataba wa hicho tunachoongea akaniambia si tatizo, mkataba utafika saa 8:00 mchana, nitapiga simu Ikulu, utaingizwa katika ndege utashuka Arusha baadaye utakimbizwa hapa haraka.

"Lakini nikamwambia mkataba huo uwe na saini tatu, moja ya huyo aliyekutuma, akaniambia haina tatizo, ya pili ya kwako Njoolai, akasema haina tatizo na ya tatu, iwe ya Yesu kwa sababu mimi ni Mkatoliki na nafanya hili kwa maslahi ya wananchi. Nahitaji Yesu ashuhudie na aweke saini," alisema Dk Slaa.

"Baada ya kumwambia hivyo, aliniacha hotelini akaondoka mbio hata ile chai aliyoninulia hakulipa ikabidi nilipe mwenyewe. Kwa hiyo nawaeleza haya wananchi kuwaonyesha uchafu na ubaya wa CCM."

Kuhusu Kambaku, Dk Slaa alimshukuru Mungu kuwa amemuonyesha kuwa ni msaliti mapema kabla ya kuingia bungeni kwani angewasiliti na kuwafanyia mabaya zaidi.

"CCM jana walisheherekea, badala ya kusikitika kwa sababu ninyi si wenzao kama walivyoniambia mimi," alisema Dk Slaa.

Alivua cheo chake cha ugombea kwa muda wa dakika tano na kuvaa cha ukatibu mkuu a chama na kumwagiza Tundu Lissu achukue hatua kali za kisheria kwa Kambaku na CCM waliomrubuni na kuwasaliti watu wa Singida Magharibi, kwani kitendo cha kumnunua mgombea ni rushwa.

Naye Tundu Lissu aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuharibu kura zao kuliko kumpigia Mohamed Misanga na kwamba hilo si kosa la jinai.

"Kura ya urais piga kwa Slaa, kura ya udiwani piga kwa Chadema lakini kura ya ubunge haribu... kama limekuja jina moja la Misanga na kama kuna jina jingine pigia hilo jingine. Kambako ametusaliti na amewasiliti kama Yuda Eskarioti alivyomuuza Yessu kwa vipande 30 vya fedha."


Chanzo: Mwananchi
 
Haya ni madai mazito. Kwani huyo Ole Njolay si yupo? Kama si kweli akanushe au aende mahakamani. Tusichotaka ni Kinana na Makamba kuanza kusema eti ni 'matusi.'

Hawa CCM wanaogopa sana kwenda mahakamani katika mambo kama haya na sababu inajulikana -- yatafumuka mengi zaidi ya hayo na kuumbuka. Si bora nusu shari kuliko shari kamili?
 
Siku zote alikuwa wapi toka 1995 kuyasema hao aje ayaseme leo? Au anayasema kwasababu anagombea urais? Angekuwa muadilifu angeyasema toka yalipotokea au angemfungulia kesi Njolay.

SLAA NI MNAFIKI WENYE HEKIMA TUMESHANGAMUA.


Kila kitu kina mahala na wakati wake wa kusemea. Mbona Jk tangu 2005 hakuwaambia watu wa kanda ya Ziwa kuwa atawaletea meli mbadala ya MV Bukoba iliyozama, hadi wakati anataka kurudi Mjengoni? Mr malaria Sugu please, tunakujua hata ukijibadili ngozi gani.
 
Hii staili ya kulipua mabomu ilimsaidia sana Lyatonga Mrema miaka ile wakati anagombea Ubunge Temeke, sina uhakika kama inaweza kusaidia sana baada ya miaka 15.

Tafadhali tuleteeni SERA MBADALA (Alternative Development Policies) na mtaona jinsi wananchi watakavyofuata kwa makundi nyuma yenu.
 
Siku zote alikuwa wapi toka 1995 kuyasema hao aje ayaseme leo? Au anayasema kwasababu anagombea urais? Angekuwa muadilifu angeyasema toka yalipotokea au angemfungulia kesi Njolay.

SLAA NI MNAFIKI WENYE HEKIMA TUMESHANGAMUA.
Acha matusi kijana. Wewe ukitukanwa utafurahi? Unajuaje kuwa Dr. Slaa ni mnafiki?
 

Umenikumbusha M.A in P.A.D.S
 
Anayepakwa matope nae hupaka wenzake matope, hii ndio siasa na upumbavu wake, kwa nini wasiongelee sera badala ya mitusi au shutuma kwa kila mgombea? Hyyetu macho.
 
umbukeni hapa JF kuna wazee na busara zao hivyo jitaahidi kupunguza matusi kadri uwezavyo hata kama ni kibaraka
 
Mpaka sasa napata wakati mgumu sana kumuelewa mtu anayeitwa Dr. Slaa. I stand to be corrected but I haven't seen or heard anything positive apart from the Scandals coming from him. Mara story za 1995, mara mishahara ya Wabunge ni mikubwa, mara CCM wamemhonga mgombea wa CHADEMA mara ooh Slaa amlipua mama Salma........ Add value to your campaigns Dr. 31 October ni karibu sana.....

Dr. Slaa if you are here please prove me wrong!
 
Anahitaji saini ya yesu! huyu jamaa anazo kweli!....au hajui anagombea urais na siyo ukuu wa kanisa katoliki..naona...ameteleza kwikwi!
Angelikuwa mgombea wa dini yako asingehitaji saini ya tatu maana kwenye dini yako kiapo kinajumuisha watu wawili tu. hahahahahahahaha
 
Anayepakwa matope nae hupaka wenzake matope, hii ndio siasa na upumbavu wake, kwa nini wasiongelee sera badala ya mitusi au shutuma kwa kila mgombea? Hyyetu macho.

Katika aliyosema DR Slaa mitusi ni ipi? Nendeni mahakamani kama viongozi wenu ni wanaume!!!
 


Kwenye red: Hiyo hiyo ndiyo value ya kampeni yake itakayowaondoa. Kama sivyo kwa nini mna hofu na anayosema? Jibuni tuhuma, au nendeni mahakamani. Halafu isitoshe Dr Slaa anafanya yote mawili -- anawakosoa hao wezi wenu wa CCM na hapo hapo anmwaga sera. Nyie CCM hamuwezi kufanya hilo la kwanza kwani wapinzani hawako katika dola hawajaiba hela za wananchi, ndo maana kosoa yenu inabakia madongo tu na mambo ya ngono na ndoa!
 


Nakuunga mkono upande mmoja kidogo! lakini 70% sikuungi mkono mkuu kwani Dr Slaa naye anajihami, anafanya kile anaachotakiwa kufanya kwa wakati muafaka. Kama ni sera anasema sana na sera zake zinaeleweka sana mkuu. Tatizo media ndo zinaegemea saaaana kwenye upupu wa shutuma. Jaribu kucheki tu mkuu likiandikwa jambo la kijinga au lolote kama shutuma utaona news zinazagaa haraka kuliko sera kamili.

Kwa hiyo wabongo bado tunasuasua sana kwenye siasa zetu, media pamoja na namna ya kujiadabisha kama hawa media group wanatakiwa kupewa sheria zinazowaongoza vizuri namna ya kuandika habari. Lakini kwa sasa ni soko holela, twende kazi mbele mbele mkuu tutashitukia tuko kwenye mstari labda.
 

Mimi nakuunga mkono 100%. Hawa CCM pamoja na matusi yao wanayoandika katika vijigazeti vyao walivyovinunua na kisha kuvisambaza bure ndiyo wanaonekana kuingiwa na hofu kubwa. Hii ya Dr Slaa inaitwa 'two-pronged assault' yaani shambulio lenye ncha kali mbili. Kukosoa na hapo hapo kutwanga sera. Wanachojua CCM ni strategy ya kutoa ahadi tu -- ambazo nyingi sana hazitekelezeki.
 
Now am tired 2 here nonsense za Dr. Slaa...hana jipya.hana sera.hana mshiko.aniniboa ile mbaya.kwa elimu yangu ndogo ya shahada toka pale mlimani inaniambia kua campaign during uchaguzis(elections) inatoa fursa adhimu ya wagombea kunadi sera zao iwe ni economic,social or development related.pia a notable scholar once said 'smart and civilized people discus issues nd facts & fools and loosers discus people' i dnt want to believe that Dr.Slaa ni looser na fukara wa sera na mshiko but am 100 pa senti convinced that anaelekea huko...mzee wangu usigeuze majukwaa ya kampeni kuwa kumbi za mipasho kama mango garden na equator glirr....by the way hivi wana JF Ph.D ya SLAA ni ya fani haswaa? Law?? Economics?? Political Science?? Finance?? Ama yake ni Divinity..sina mbavu
 
Watu wengine bana, kazi kwelikweli.

Yaani unaona maneno mawili matatu ya shutuma na unaamini kuwa ndiyo hotuba nzima ya Slaa?

Kama Slaa asingeliyasema hayo, basi wala wasingelimuandika. Kama huamini basi angalia hotuba za Lipumba.

Ndiyo maana magazeti ya udaku yanauzika. Usipochanganya udaku na Sera basi huandikwi na huongelewi.

Kama mnataka SERA za CHADEMA si ziko hapahapa JF? Kwa nini usisome?

Au wataka Slaa pia akuahidi kuwa atawanunulia wake zenu na nyumba ndogo zenu amhhhhh amhhhhh......... upppsss!!!

Mungu kawajalia UBONGO ila nyie mnautumia kisivyo, ovyooooo kabisaaaaa!!!!!!......

Mchagueni Kikwete na atakununulieni MELI pale Dodoma. Train za umeme ziwa Tanganyika na Nyanza/Nyasa.
Atawajengea Dubai mbpyaaa pale Kigoma. Mwaka 2015 wakati anaondoka, Kigoma itakuwa kama picha chini............


 

Umenena my friend. Huwezi kumwaga sera bila ya kueleza sera za mwenzako zimetufikisha hapa tulipofika -- kwenye wizi mkubwa wa mali za wananchi. Ukitoa sera bila kugusia hayo, basi huna maana ya kuitwa mpinzani mwenye nia ya kuwa-replace hao wezi. Lazima useme waliiba nini, lini, wapi n.k. -- na jamani siyo matusi hayo, ni tuhuma tu, mwenye kuumwa aende mahakamani kama wanavyosema baadhi ya wenzangu waliotangulia.
 

usilopoke wewe fuatilia mambo ujue unahitaji kufanya uchunguzi kwanza wewe!!
 
Karibu sana JF.
Tatizo lako ni ELIMU NDOGO YA UDSM kama ulivyosema na hujatembea. Masikini kijana wa watu, poor you!!!! Na kama huna mbavu ndiyo kabisaaa, hata uwezo wa kufikiri huna.
Walikuwepo akina August na sasa wanaanza kuingia akina SEPTEMBER. Mwaka huu wataingia kwa majina mengi sana ili wapige kura ya maoni na Kikwete ashinde. So far ana-tail nyuma sana ya Dr wa kweli.
 

Ungekuwa karibu ningekuambia gonga. Lakini umesahau fly-overs muungwana alzoahidi kwa Dar! Wee Bwana wee nchi hii itakuwa min-US in 5 years na Watanzania eti wanaamini! Miafrika ndivyo ilivyo kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…