Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Dk Slaa awalipua Pinda, Mkapa
Salim Said, Singida
MGOMBEA kiti cha urais kupitia Chadema, Dk Willibrod Slaa amemlipua Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisema kuwa akiwa mwenyekiti wa kikao cha kamati ya wabunge wote alimtaka ajitokeze mbele ya wabunge na akanushe kuwa hakutaja kiwango cha mishahara ya wabunge bali magazeti yalimnukuu vibaya.
Dk Slaa amekuwa akieleza kila mara kuwa wabunge wanalipwa mshahara mkubwa tofauti na hali halisi ya uchumi wa nchi na akatamka bayana kuwa watunga sheria hao wanalipwa zaidi ya Sh7 milioni, jambo ambalo alisema ni kufuja fedha za walipa kodi.
Jana kwenye mikutano ya kampeni ya hadhara aliyoifanya katika kata za Igilansoni na Sepuka kwenye Jimbo la Iramba Magharibi jana, Dk Slaa alielezea jinsi msimamo wake ulivyoitingisha serikali na madai kuwa Waziri Pinda alijaribu kumtaka akane kauli yake iliyonukuliwa na vyombo vya habari.
"Nilikataa nikamwambia waziri mkuu kuwa kama mnakataa mshahara wa mbunge si Sh7 milioni, tangazeni kima halisi cha mshahara wa wabunge katika gazeti ili Watanzania wajue," alisema Dk Slaa.
"Lakini waziri mkuu alikataa na kuniomba nisiendelee kulitangaza suala hilo kwa wananchi kwa madai kuwa nawagombanisha wabunge na wapigakura wao.
"Lakini sikumsikiliza kwa kuwa natetea haki ya Watanzania na hivyo niliamua kutoka pamoja na baadhi ya wabunge wenzangu wa Chadema na kupita mikoa mbalimbali kuwatangazia wananchi tofauti hiyo ya mishahara kati ya wabunge na watumishi wa umma."
Dk Slaa aliendelea kusema: "Wakasema watanishitaki nikawambia kama mshahara wao ni siri, wa kwangu sio siri na mimi nilitangaza wa kwangu... kwa kuwa wananchi si wajinga wanajua kuwa kwa kuwa Slaa ni mbunge na Mohammed Misanga ni mbunge, basi kima chao kinalingana."
Dk Slaa alimgeukia rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akimtuhumu kuwa alimtumia mpwa wake, Ole Njolai kwenda kumuhonga ili aache ubunge wa jimbo hilo mara baada ya kuihama CCM 1995. Dk Slaa alikuwa mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema kwa vipindi vitatu.
"Aliniita hotelini Karatu na kuniambia nimetumwa na Rais Mkapa; kama unataka ubalozi, kama unataka kwenda Umoja wa Mataifa (UN) utapata au kama unataka fedha sema ni shilingi ngapi unataka ili uache ubunge na urudi CCM," alisema Dk Slaa.
"Nikamwambia nahitaji mkataba wa hicho tunachoongea akaniambia si tatizo, mkataba utafika saa 8:00 mchana, nitapiga simu Ikulu, utaingizwa katika ndege utashuka Arusha baadaye utakimbizwa hapa haraka.
"Lakini nikamwambia mkataba huo uwe na saini tatu, moja ya huyo aliyekutuma, akaniambia haina tatizo, ya pili ya kwako Njoolai, akasema haina tatizo na ya tatu, iwe ya Yesu kwa sababu mimi ni Mkatoliki na nafanya hili kwa maslahi ya wananchi. Nahitaji Yesu ashuhudie na aweke saini," alisema Dk Slaa.
"Baada ya kumwambia hivyo, aliniacha hotelini akaondoka mbio hata ile chai aliyoninulia hakulipa ikabidi nilipe mwenyewe. Kwa hiyo nawaeleza haya wananchi kuwaonyesha uchafu na ubaya wa CCM."
Kuhusu Kambaku, Dk Slaa alimshukuru Mungu kuwa amemuonyesha kuwa ni msaliti mapema kabla ya kuingia bungeni kwani angewasiliti na kuwafanyia mabaya zaidi.
"CCM jana walisheherekea, badala ya kusikitika kwa sababu ninyi si wenzao kama walivyoniambia mimi," alisema Dk Slaa.
Alivua cheo chake cha ugombea kwa muda wa dakika tano na kuvaa cha ukatibu mkuu a chama na kumwagiza Tundu Lissu achukue hatua kali za kisheria kwa Kambaku na CCM waliomrubuni na kuwasaliti watu wa Singida Magharibi, kwani kitendo cha kumnunua mgombea ni rushwa.
Naye Tundu Lissu aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuharibu kura zao kuliko kumpigia Mohamed Misanga na kwamba hilo si kosa la jinai.
"Kura ya urais piga kwa Slaa, kura ya udiwani piga kwa Chadema lakini kura ya ubunge haribu... kama limekuja jina moja la Misanga na kama kuna jina jingine pigia hilo jingine. Kambako ametusaliti na amewasiliti kama Yuda Eskarioti alivyomuuza Yessu kwa vipande 30 vya fedha."
Chanzo: Mwananchi