Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amesema hakuna Mtanzania anayemchukia Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ila malalamiko yao dhidi yake ni kutaka kujua ukweli kuhusu mambo yanayomhusu.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana, wakati akitoa maoni kuhusu kauli ya Mkapa aliyotoa mkoani Iringa Jumapili iliyopita, akiwaonya wanasiasa kuacha fitina, chuki, majungu, udini na ukabila kwa hofu kwamba nchi inaweza kuingia katika machafuko.
Mkapa alinukuliwa na vyombo vya habari jana akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Walolesi la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa alipokaribishwa na Askofu Dayosisi hiyo, Dk Owdenburg Mdegella kuwasalimia waumini.
Dk Slaa pia alimtaka Askofu Mdegella kuwaomba radhi Watanzania kwa kitendo chake cha kumtetea na kumsifu Mkapa. Alisema kwa kitendo kama hicho makanisa yanaweza kufika pabaya, kwa kurukia mambo na kusifu watu wakimezea mate michango ya fedha.
"Hatumchukii Mkapa, hakuna mtu anayemchukia, yeye ni rais mstaafu, tunachotaka ni kuwa aache blaablaa za kupotosha hoja. Anachofanya ni kujaribu kupoteza muda na kuwapamba wananchi wasahau hoja ya msingi iliyopo sasa," alisema Dk Slaa.
Dk Slaa ambaye pia ni mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema alisisitiza kuwa, hakuna chuki dhidi ya rais huyo mstaafu zaidi ya kutaka kujua iwapo alifanya biashara alipokuwa Ikulu kama rais wa Tanzania.
"Sisi hatumchukii ila tunataka kujua ukweli, kama alipokuwa Ikulu, akiwa Rais wa taifa hili alifanya biashara na kuuza mali ya Watanzania. Tunataka atueleze kama kampuni iliyonunua Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira ni yake, mkewe, watoto wake na rafiki yake Yona au la?" alihoji Dk Slaa.
Aliongeza kuwa, wananchi wa Tanzania wanataka kusikia kauli ya rais huyo mstaafu, kwa kuwa mgodi wa Kiwira ulikuwa ni mali yao kabla ya kuuzwa.
"Hayo ndiyo tunayotaka kusikia kwa faida ya wananchi, kwani ni haki kujua," alisema Dk Slaa.
Alifafanua kuwa Mkapa anapaswa kuwaambia wananchi kama tuhuma zinazomkabili ni kweli au uongo na kwamba, akithibitisha ni uongo ni vema, lakini ikiwa ni kweli basi sheria ichukue mkondo wake badala ya kuendeleza maneno aliyoyaita blaablaa ambazo hazitamsaidia.
Alisema kuwa siasa za chuki, majungu, fitina, ukabila na udini anaozungumzia Mkapa utaisha pale atakapowaweka wazi Watanzania kuhusu tuhuma zinazomkabi.
"Hizo siasa za chuki, majungu, fitina, ukabila na udini zitaisha akiwaweka wazi Watanzania juu ya umiliki wa Mgodi wa Kiwira. Zaidi ya hayo nashangaa kwa nini azungumzie hayo wakati huu anapokabiliwa na tuhuma za kufanya biashara Ikulu," alisema Dk Slaa.
Akizungumzia hatua ya Askofu Mdegella kumtetea Mkapa na kueleza kuwa anazushiwa uongo na vyombo vya habari, Dk Slaa alisema askofu huyo amewakosea Watanzania na anapaswa kuwaomba radhi.
"Yule Askofu wa Iringa aliyemtetea Mkapa kuwa anazushiwa, lazima awaombe radhi Watanzania, kwa sababu amewakosea," alisema Dk Slaa.
Alifafanua kuwa anayepaswa kujisafisha mwenyewe mbele ya watu aliowaongoza ni Mkapa na si askofu huyo.
Alisema hatua ya askofu huyo na viongozi wengine wa dini hasa makanisa si sahihi, kwani inaendeleza utaratibu wa zamani wa kutomwonya au kumwambia ukweli mkubwa anapokosea.
"Baba kutoambiwa akikosea hiyo ni tabia ya zamani na mbaya, haifai katika ulimwengu wa leo. Tabia ya baba kutosahihishwa ndiyo imetufikisha hapa tulipo," alisema Dk Slaa.
Alisema anawaheshimu viongozi wa dini, lakini akaonya kuwa wasiingie mahali pabaya kwa kusifu watu kwa sababu ya kuhitaji michango makanisani.
"Viongozi wa dini tunawaheshimu, wasiingie mahali pabaya na kusifu watu kwa sababu ya kutaka michango ya harambee. Kama hawajui kitu bora, wanyamaze, vinginevyo watalifikisha kanisa pabaya. Sisi tunawategemea wao wawe safi, lakini hii inatia hofu juu yao," alisema Dk Slaa
Source:Mwananchi