Elections 2010 Dk Slaa on Clouds FM

Hongereni Clouds kwa kujipatia wasikilizaji weeengi....wakati mnamuhoji Dr Slaa,
Jamaa ameonesha ukomavu kweli kwani kila hoja ama swali lililoulizwa amalijibu kiufasaha na amezidi kuonyesha kuwa katika mazungumzo si mtu ambaye anaandaliwa hotuba na kuwasomea watu majukwaani bali anajua anachokisema, anachotaka kukifanya akiwa rais.
Mtu asiyehofu maswali ama kuzungumzia yale anayoyaamini. To top everything up He has guts!
Watzanania tunahitaji nini zaidi? Huyu ndiye anayetufaa!
 

hauna hoja yoyote ya msingi
 

hauna hoja yoyote ya msingi
 
Daaaaaaaaaaah sijapata kuona interview bomba kama hii tena kupitia clouds, Dr Slaa yuko makini, hizi sera anazozieleza Tanzania tutakuwa kama ulaya mi nakuambia, mambo ni mengi sana na uwezo wa Tanzania kuwapa wananchi wake maisha bora unawezekana, mi nimependa jinsi CHADEMA watakavyo:-

1. Punguza ukubwa wa serikali.
2. Kutoa elimu na afya bure.
3. Kufumua mikataba ya madini na maliasili nyingine ili tuweze kupata mirahaba minono kwa rasilimali zetu.
4. Kuchagua mawaziri ambao si wabunge kwani watakuwa kweli waadilifu na kutenda kazi bila ubabaishaji.
5. Kupunuguza matumizi ya serikali kama kununulia mashangngi, kununulia dhamani za kifahari na hata kujenga mijumba ya kifahari.
6. Kuhakikisha nyumba za serikali zilizouzwa zinarudi serikalini.
7. Kupambana na ufusadi na kurudisha hela zilizoibwa na hao mafisadi kwa manufaa ya wananchi wote.
8. Kupunguza mfumuko wa bei, bei za umeme na mafuta ya mitambo kama petrol nk.

Ni mengi ila Tumchague Dr Slaa kwani tunahitaji mabadiliko na bila mabadiliko nchi hii tutaendelea kudidimia kabisaaa.
 
Naomba msaada wenu wandugu station ya Clouds FM inapatikana kwenye mita bendi ngapi???????????
 
Slaa ameitumia nafasi ya leo vizuri sana.. sbb alikuwa short,direcct to the point. na hakuwa akiuma uma maneno.
Binafsi nawapongeza Clouds, Hando na Babra wamejitahidi sana kuwawakilisha wasikilizaji wao vzr
 
Naomba msaada wenu wandugu station ya Clouds FM inapatikana kwenye mita bendi ngapi???????????

Mkuu Gwallo, haya masafa ya FM yanategemea uko mkoa gani hapa tz.. ila kwa Dar ni 88.4
 
Mbali na matangazo kuwa mengi,Dr. Slaa ameeleza vizuri mno maswala yote yaliyohitaji kupata ufafanuzi. BIG UP HANDO, WELL DONE CLOUDS...CHADEMA JAMANI KWA AJILI YETU NA VIZAZI VIJAVYO.MUNGU AKUTANGULIE DR. Slaa.
 
Kamarade, unaota ukiwa mbele ya kompyuta yako.

Huu upupu wenzako Makamba & co. wameshindwa kumchafua Dr. Slaa.

Wewe endelea tu kuota sisi tunasonga!!!
 
WaJF mimi naamini dakta ni kichwa tuachane na propoganda za wachafuzi. Jamaa anajua kuchambua, anajua matatizo yaliyopo na amejiandaa kuyafanyia kazi. Tauchane na ushabiki. Hivi kujenga barabara, matundu ya vyoo, mashule, vivuko, kuwaripa mikopo ya vyama vya ushirika ni sera? HAPO UNATEKELEZA WAJIBU WAKO NA KUNA WATU WANAOHUSIKA NA HIVI VITU WANALIPWA KWA KODI ZETU. Hivyo sera ni elimu bora, miundombinu bora, maisha bora hapa sasa ndiyo unacover vilikorokoro vyote vinavyosemwa kimojakimoja kuwa ni sera. DAKTA NAMPA ONGERA SANA AMEJIELEZA VIZURI SANA. NADHANI CLOUDS LEO IMESIKILIZWA VILIVYO. TUWAPE ONGERA KWA HILO ATLEAST KUMLETA NA WATU WENGI WAKAMSIKIA WAKIWA NA FRESH MIND UNAJUA TENA ASUBUHI.
 
Mbali na matangazo kuwa mengi,Dr. Slaa ameeleza vizuri mno maswala yote yaliyohitaji kupata ufafanuzi. BIG UP HANDO, WELL DONE CLOUDS...CHADEMA JAMANI KWA AJILI YETU NA VIZAZI VIJAVYO.MUNGU AKUTANGULIE DR. Slaa.


Jamaa watakuwa wametengeneza hela kweli maana wanajua wengi leo wangesikiliza.
 
muda si mrefu dk slaa ataanza kurindima kupitia redio ya watu. Hebu tuone hawa jamaa wameandaa vipi huu mdahalo.

Kwa hili pia nawapongeza clouds

audio (kwa hisani ya mfunyukuzi - jf member)



mbona hiyo audio haipo jamani, tupeni uhondo ulioridima huko mawingu
 
Last edited by a moderator:
Unajua kama wewe ni msafi hutakua na hofu ya kwenda mbele ya media mungu yu p1 nae cc ha2na dola,serikali,fedha but kadi ze2 ndo rungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…