Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika Jimbo jipya la Uyole, mkoani Mbeya.
Dk. Tulia ametua jijini Mbeya muda mfupi uliopita na kukabidhiwa fomu hiyo na Justine Mwansepele, ambaye alikuwa ameichukua kwa niaba yake kama mwakilishi wa Tulia.