PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Dkt. Tulia Ackson, leo Disemba 19, 2025, ameifuta machozi ya familia ya Emmanuel Julius Kyanula kutoka kata ya Igawilo, Uyole, ambayo ilipata janga la nyumba kuungua kwa moto.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha msaada huo, Dkt. Tulia Ackson amekabidhi mabati (bando 5), misumari pamoja na chakula kwa familia hiyo, ambapo mama wa familia ndiye aliyepokea msaada huo kwa niaba ya familia.
Dkt. Tulia pia amewashukuru wananchi wa mtaa wa Mponja, kata ya Igawilo, ambao walishirikiana na familia hiyo tangu mwanzo wa janga hilo kwa kutoa misaada mbalimbali, ikiwemo hifadhi ya muda ya kuishi na mahitaji mengine muhimu.
Aidha, Spika mstaafu huyo amemuongezea mtaji mama wa familia hiyo ambaye ni mfanya biashara ya "Mama Ntilie Ilo" ili kuweza kuinua kipato cha familia, hatua hii ikiwa msaada muhimu kufuatia ajali iliyomkuta baba wa familia, Bwana Emmanuel Kyanula, aliyepata kuvuja mguu.