Dk. Willbrod Slaa: Tutapeleka mapendekezo yetu ya Katiba mpya kwa lori

Dk. Willbrod Slaa: Tutapeleka mapendekezo yetu ya Katiba mpya kwa lori

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,503
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefunga rasmi mikutano yake ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Rasimu ya Katiba mpya kupitia mabaraza huru ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

Chama hicho kimesema kimefanikiwa kukusanya maoni ya wananchi milioni tano na kwamba wanatarajia kupeleka maoni hayo kwenye ofisi za Tume kwa lori kwa kuwa ni mengi.

Akifunga mikutano hiyo juzi jijini humo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alisema katika mikutano 49 waliyoifanya ndani ya mikoa tisa nchini, wamekusanya takribani maoni milioni tano kutoka kwa Watanzania kuhusu maboresho ya rasimu hiyo dhidi ya milioni mbili yaliyokusanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa wanachama wake.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo juzi katika viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, wakati akihitimisha mkutano wake wa mabaraza huru ya kukusanya maoni kwa Watanzania juu ya Rasimu ya Katiba mpya. Alisema, Chadema wanaunga mkono Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, lakini wanapingana naye katika baadhi ya vipengele kama vile Tanzania Bara kuitwa Tanganyika.

Baadhi ya wananchi waliokuwapo kwenye mkutano huo walipendekeza kuongezwa kwa vipengele vya haki kwenye tunu za taifa.

Tunu saba za taifa ambazo zimependekezwa katika rasimu hiyo ni utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya taifa.

Wananchi hao walipendekeza kwamba kwenye rasimu hiyo kiongezwe kipengele kinachomruhusu kila Mtanzania kuwa na haki ya kumiliki ardhi, kupata huduma bora za afya kama viongozi wa serikali na wabunge wanavyofanyiwa.

Dk. Slaa alisema katika mikutano hiyo wamezunguka katika mikoa tisa na kufanya mikutano 49 huku zaidi ya Watanzania milioni tano wakiwa wametoa maoni yao juu ya rasimu hiyo.
Kwa hisani ya Nipashe
 
Akifunga mikutano hiyo juzi jijini humo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alisema katika mikutano 49 waliyoifanya ndani ya mikoa tisa nchini, wamekusanya takribani maoni milioni tano kutoka kwa Watanzania kuhusu maboresho ya rasimu hiyo dhidi ya milioni mbili yaliyokusanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa wanachama wake.
CCM hawawezi kuongea kuhusu katiba mpya wasiliseme neno CHADEMA na CHADEMA nao vile vile hawawezi kuongea kuhusu katiba mpya wasiliseme neno CCM kana kwamba kinachotafutwa ni ushindi dhidi ya mapambano ya vyama vyao katika kuuza sera na ilani ya uchaguzi wakati kinachotafutwa kwa sasa na wapenda maendeleo wasio wabinafsi ni maisha bora kwa Watanzania kwa vizazi vijavyo.

Kinachofanyika kwa sasa kati ya hivi vyama ni kufanya kazi kwa kuviziana, kupigana vijembe na spinning hata katika maswala ambayo ni muhimu sana for generation to come.

Ni huzuni na masikitiko kwa jambo la kitaifa kwa sasa kugeuzwa kuwa ni swala la vyama vya siasa huku wananchi wakiwa fuata upepo.

Vyama vya CCM, CHADEMA na CUF haviwatendei haki wananchi wanaovipatia pesa kila mwezi kwa njia ya ruzuku. Kwa pesa za wananchi, hivi vyama vinatumia hizo nguvu kusukuma pembeni mawazo ya taasisi, Asasi na makundi mengine ya wananchi yasisikite katika kutoa mawazo na maoni yao katika uboreshaji wa Rasimu ya Katiba.

Kwa nguvu hizi vya vyama vya siasa, siyo ajabu kitakachopatikana 2015 ndani ya katiba mpya ni sera na ilani ya uchaguzi ya chama kimoja kati ya hivi vitatu, badala ya mawazo na mwerekeo wa wananchi wote kwa kizazi hiki na kijacho.
 
Nakumbuka mfalme wa porini alikaririwa kua kavunja record kwa kukusanya tu maoni ya watu Mil 2,Tanzania yote

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nakumbuka mfalme wa porini alikaririwa kua kavunja record kwa kukusanya tu maoni ya watu Mil 2,Tanzania yote

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Mkuu tembo milioni 2 ni wengi sana..si wataisha??
 
Kwa hiyo slaa hafanyi uchambuzi hata yale ambayo yametolewa kwa kufanana na kujirudia yeye anapeleka yote bila hata kuchambua,wenzake ccm walichambua kwanza kweli chadema ni janga la taifa hili.
 
Wasije tu akawa kama mzee wa kiraracha
 
Kumiliki ardhi? ... kila mtanzania anamiliki ardhi.
 
Kwa nguvu hizi vya vyama vya siasa, siyo ajabu kitakachopatikana 2015 ndani ya katiba mpya ni sera na ilani ya uchaguzi ya chama kimoja kati ya hivi vitatu, badala ya mawazo na mwerekeo wa wananchi wote kwa kizazi hiki na kijacho.

Unorganised and civic incompetent citizens like Tanzanians CAN NOT avoid being ruled by organized groups....
Kama watanzania wamejengewa mazingira ya kuwaogopa mabalozi wa nyumba kumi, watakuwaje na uwezo wa kujadili katiba bila kutiwa hamasa??
Nami nilitaka iwe kama ulivyosema, LAKINI si kwa Tanzania hii ambayo watu tu waoga wa kutiliwa mifano!
 
Kwa hiyo slaa hafanyi uchambuzi hata yale ambayo yametolewa kwa kufanana na kujirudia yeye anapeleka yote bila hata kuchambua,wenzake ccm walichambua kwanza kweli chadema ni janga la taifa hili.

Pole. Maoni ya Wanachama wa CHADEMA hayatachakachuliwa. Yatawasilishwa kama yalivyo. Hiyo mizigo itakayowasilishwa ni ushahidi wa hao wananchi mamilioni walioshiriki Mabaraza ya Katiba ya CHADEMA.
 
Aongeze na haya,

1. Yale maoni,maamuzi,tathimini na Dira ya Dr. Mipango wa tume ya mipango yahaririwe na kuwa sehemu ya katiba.

2. Muundo wa Serikali zote uwe ni shirikishi kwa vyama vyote kulingana na ushindi wao kwenye uchaguzi.(Mseto)

3.Slogan ya (kisiwa cha amani) ibadilike na kuwa na slogan ya kimaendeleo zaidi kama vile "Taifa bora la weusi" kwa kuwa neno aman lina tumika kutupumbaza.

4. Ulezi wa watoto hadi miaka 18 ufuatiliwe kwa karibu sana kuanzia serikali kuu mpaka mtaa yani wawe ni kipande cha serikali kama jeshi kwa ajili ya kizazi imara kijacho.

5.Katiba itaje,itambue uwepo wa wiki maalumu ya kuenzi na kusherekea utamaduni wa Taifa letu kutoka makabila na matabaka yetu.
 
Back
Top Bottom