Dkt. Abbas afanya ziara TAFORI, ahamasisha watafiti kufanya tafiti za kimaendeleo

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Na Mwandhishi Wetu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas amewahamisisha Wataalamu wa utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), kuandaa miradi mbalimbali ya utafiti yenye kuleta maendeleo chanya ndani ya Taasisi na katika sekta ya Misitu na ufugaji Nyuki.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Menejimenti ya Utumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) hii leo Januari 24, 2025 wakati alipofanya ziara yake katika Taasisi hiyo kwaajili ya kuipongeza Taasisi kwa mchango mkubwa wanaoutoa kupitia shughuli za kiutafiti na kusikiliza changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo.

Alisema, ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za Taasisi ni vyema kwa Taasisi kupitia wataalamu wake ikaanda miradi ya kimkakati yenye kuleta maendeleo kwenye Taasisi na katika sekta ya Misitu na ufugaji Nyuki ili kukuza pato la Taifa.

Dkt. Abbas alisema, Taasisi kupitia watafiti wake inahaja ya kuongeza uzoefu kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Misitu na ufugaji Nyuki ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi na Mamlaka zilizoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa kufanya ziara mbalimbali ili kupata ujuzi na maarifa utakaoongeza ufanisi katika utendaji kazi ndani na nje ya Taasisi.

Alisema, Taasisi inatakiwa kuwekeza katika mashamba makubwa ya Misitu yatayotumika kwa ajili ya shughuli za kiutafiti na kuweza kuanzisha biashara zitakazoleta maendeleo katika Taasisi na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Katibu Mkuu ameitaka TAFORI kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi hapa nchini kwa kutoa elimu na mafunzo kupitia tafiti wanazozifanya katika sekta ya Misitu na ufugaji Nyuki.
 
Oh!! umefika huko 🤣 🤣 🤣
Una bahati title imehaririwa.

Sasa tuwakumbusheni kuwa kuhamasisha watu kutenda wanalopaswa kutenda imetosha. Tunataka vitendo na maendeleo.

Yaani Taasisi yenye majukumu ya kufanya tafiti kupitia miradi mbalimbali nayo ni ya kukumbushwa/ kuhamasishwa kufanya hivyo tena?😂
 
Ukiwa hujavuta bangi kama kawaida yako uje tujadiliane vizuri.
 
Hili boya kipindi cha magu lilikuwa linapenda sifa sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…