Dkt. Abbass: Kiuchumi tuko vizuri ndio maana hatujashusha mishahara ya watumishi kama nchi nyingine

Dkt. Abbass: Kiuchumi tuko vizuri ndio maana hatujashusha mishahara ya watumishi kama nchi nyingine

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema, Serikali haijaacha kuwalipa watumishi wake katika kipindi hiki cha #CoronaVirus kwa sababu iko vizuri kiuchumi

Ameongeza, “Nchi jirani zimepunguza mishahara lakini kwa Tanzania watu bado wanapata mishara yao tena kwa wakati bila kusheleweshwa”

Amebainisha “Corona imegusa sana uchumi na sekta nyingine mbalimbali lakini hatua tulizochukua kama Tanzania zimetuweka katika nafasi nzuri na kulinda uchumi wetu”

Amesema maambukizi ya #CoronaVirus yamepungua sana, Watu wengi wanapima na amebainisha kuwa takwimu zinaonesha Wagonjwa hawafiki 60 kwa Tanzania

Aidha, vipimo vya sasa vikitoa majibu vinaaminika zaidi kuliko vile vya awali ambavyo vilitoa majibu ya Mapapai na Mbuzi wakiwa wameathirika na virusi hivyo

Amemalizia, “Nchi nyingi zimebadili mkakati wa utoaji taarifa, nyingi zimeacha kutoa taarifa za COVID19. Tumebadili sababu tunaamini Watanzania wameelewa lakini pale kwenye umuhimu tutaendelea kukumbushana”

Yuko Live Clouds FM wakati huu
 
Bia yetu ni taasisi?
Naona yuko macho 24/7 na kila uzi mpya lazima akoment ndani ya 10 bora sijui anatrace vipi nyuzi zote mpya au ndiyo UNRead

Vuneni hela vijana uchaguz ukiisha hamtapata hela.
 
Dkt. Hassan Abbas amesema, Serikali haijaacha kuwalipa watumishi wake katika kipindi hiki cha #CoronaVirus kwasababu iko vizuri kiuchumi
ALHAMDULILLAAH. ENDELEENI NA MOYO HUO HUO. KUWAJALI WATUMISHI WA UMMA NI KTK KUJALI MAISHA YA RAIA KWA UJUMLA.
 
S
Mungu kwanini hawa wajinga wasipoteze hata mmoja mmoja ili watueleze ukweli.
Serikali ndio iliyo waajiri? Yaani tuanze kuwaza watu walio jiajiri wenyewe. Inamaana ukisema tuwalipe walimu wa private maana yake tuwalipe na wafanyakazi, wengine wote wa makampuni ya private hizo pesa tunaokota ama. Hatulipilipi hovyohovyo tunaenda kwa mahesabu. Hao walimu wa private wakipata faida huwa wanaipa serikali asilimia ngapi na wenye hizo shule je huwa wanaipatia serikali asilimia ngapi? Tumia akili mkuu usitumie hisia.
 
Kwa hio bado hatujafikia kua donor country sio?

Maana dona Countries zimewabeba mpaka wafanyakazi wa Private Sectors.
 
Bia yetu ni taasisi?
Naona yuko macho 24/7 na kila uzi mpya lazima akoment ndani ya 10 bora sijui anatrace vipi nyuzi zote mpya au ndiyo UNRead

Vuneni hela vijana uchaguz ukiisha hamtapata hela.
Ni kijana wa b7 fc...wazee wa kusifu na kusujudia ili mkono uende kinywani
 
Wenzenu wameongeza 100% ya salary wewe unazungumzia habari ya kutokushusha.
IMG-20200529-WA0002.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom