Dkt. Albina Chuwa, Kauli yako kuhusu kupungua kwa umaskini ni kejeli kwa Watanzania

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Amesema Dkt Albina Chuwa Mkurugenzi wa Takwimu. ameyaongea juzi tarehe 17/ 02/ 2020, Ninamnukuu;

“Hali ya umaskini wa kipato hapa nchini Mwaka 1991-92 ulikuwa Asilimia 39, 2007 umaskini ulikuwa asilimia 34, 2012 Asilimia 28.4 na 2018 hali ya umaskini likuwa 26.4, kasi ya kupungua umaskini hapa nchini inaenda kwa mwendo wa kasi”

Full text iko hapa:
Swali:
Umaskini unapungua vipi wakati soko la bidhaa za nje limekufa? Ajira katika sekta binafsi zinakufa? Serikali imeshindwa kuajiri miaka 5? Mshahara bado watu wanapata aliouacha Kikwete?, Umaskini unapungua kwa maskini vipi? Wapambe mnampotosha Rais.

Wahitimu wako mitaani bila ajira, wakulima wa korosho kule Mtwara wamedhulumiwa pesa zao, wafanyabiashara wanaofunga biashara zao kila uchao, umasikini unapunguaje?
 
Wauza mihogo uswahilini wanafunga biashara, maduka yanafungwa,wauza vitumbua wanafunga biashara,mafundi ujenzi wamerudi vijijini.Sijui tafit alizifanyia wapi?
 
Omba ABC za uchumi kutoka kwa wachumi wakueleze vipimo/viashiria vya kupungua umasikini ni vipi ,hivyo ulivyotaja hata kimoja hakihusiki.

Nakupa mwangaza tu:
1. Kuongozeka kwa pato ghafi la taifa yaani Gross Domestic Product(GDP)

2. Ukuaji wa sekta isiyo rasmi yaani ujasiriamali

3. Uzalishaji viwandani na mashambani kuongezeka. Takwimu zinajieleza.
 
Inawezekana asilimia za masikini zikapungua, lakini masikini wakaongezeka.

Kwa sababu, asilimia za masikini mwaka 1992 zinaendana na idadi ya watu wa mwaka 1992, na asilimia za masikini za 2020 zinaendana na idadi ya watu ya mwaka 2020.

Ingekuwa vizuri kama tungeongelea idadi ya masikini, si asilimia ya masikini.

Asilimia ya masikini katika nchi yenye population growth ya 3% inaweza kuficha uhalisi wa kuongezeka umasikini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Omba ABC za uchumi kutoka kwa wachumi wakueleze vipimo/viashiria vya kupungua umasikini ni vipi ,hivyo ulivyotaja hata kimoja hakihusiki.

Nakupa mwangaza tu:
1. Kuongozeka kwa pato ghafi la taifa yaani Gross Domestic Product(GDP)

2. Ukuaji wa sekta isiyo rasmi yaani ujasiriamali

3. Uzalishaji viwandani na mashambani kuongezeka. Takwimu zinajieleza.

1. Kuongozeka kwa pato ghafi la taifa yaani Gross Domestic Product(GDP)
Kwa GDP gani iliyokuwa kwa miaka hii ya Jiwe 2016- 2019. Nchi imekalia kutengeneza data tu za kujidanganya. GDP iliyokuwa utaiona hata kwa kutumia HDI (human Development Index), yaani kuboreka kwa huduma za jamii; barabara, elimu, afya. Hii ya Dr Albina Chuwa kuiona mpaka ujiondoe akili

2. Ukuaji wa sekta isiyo rasmi yaani ujasiriamali
Sekta isiyo rasmi kuna members hapo juu wamekujibu kuwa hata wauza mihogo wanafunga biashara, wewe mwenzetu unaipimaje?

3. Uzalishaji viwandani na mashambani kuongezeka. Takwimu zinajieleza.
Korosho ambalo ndilo zao linaloongoza kwa kuleta fedha za kigeni lilisambaratishwa mwaka 2018 baada ya JESHI kuamriwa kubeba. Kuna watu mpaka leo wanadai hawajalipwa
 
Chuwa kwanza ulipata karai kwenye chemistry, na statistics. Kuwa Director General ni ngekewa tu. Leo umesahau kuwa na wewe ni third class citizen
Amesema Dkt Albina Chuwa Mkurugenzi wa Takwimu. ameyaongea juzi tarehe 17/ 02/ 2020, Ninamnukuu;

“Hali ya umaskini wa kipato hapa nchini Mwaka 1991-92 ulikuwa Asilimia 39, 2007 umaskini ulikuwa asilimia 34, 2012 Asilimia 28.4 na 2018 hali ya umaskini likuwa 26.4, kasi ya kupungua umaskini hapa nchini inaenda kwa mwendo wa kasi”

Full text iko hapa:
Swali:
Umaskini unapungua vipi wakati soko la bidhaa za nje limekufa? Ajira katika sekta binafsi zinakufa? Serikali imeshindwa kuajiri miaka 5? Mshahara bado watu wanapata aliouacha Kikwete?, Umaskini unapungua kwa maskini vipi? Wapambe mnampotosha Rais.

Wahitimu wako mitaani bila ajira, wakulima wa korosho kule Mtwara wamedhulumiwa pesa zao, wafanyabiashara wanaofunga biashara zao kila uchao, umasikini unapunguaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli nimemsikiliza huyu Mama. Inawezekana data ni za kupika .... yaani Tanzania, umaskini uko chini kuliko South Africa. Duh, sasa ni nini kunatufanya tusiwe kwenye uchumi wa kati ....!!?

Hivi Watanzania wamejifunzia wapi kusifia kiasi hiki ... Yaani watu wanapopewa jukwaa ni mwendo wa kusifia mpaka aibu. Sijui akina Mwinyi, Mkapa na JK wanajisikiaje wanapoalikwa kwenye hafra za Mheshimiwa. Ninekuwa ni mimi ningekuwa nawambia leo sikuamka vizuri ili kukwepa ....!!
 
Wenye mamlaka na Viongozi wetu ni kama Manabii, wanaongea wanachoamini wao na sisi Wananchi/Waumini wao kazi yetu kuamini.

Utasikia kanyageni mafuta kila kitu kitakuwa sawa....msiulize kivipi, nyie kanyageni.
 
Hivi hamuoni mpaka wametunga na sheria kabisa kuhalalisha uongo wao?

Hawa binaadam sio wa kawaida hawa.

Katika hali ya kawaida, baada ya kuweka uongo huo, wataalam mbalimbali wangejitokeza kuuchambua na kuupinga.

Sasa hivi ukijitia mjuaji unaishia kupewa kesi ya uhujumu uchumi.

Hili ndilo taifa wanalojenga hawa wazalendo.
 
Ila kwa huu uwongo wanaoutoa kwa kumuogopa Jiwe iko siku watawajibika na Shahada zao zitakuwa challenged.
 
Kwa kweli nimemsikiliza huyu Mama. Inawezekana data ni za kupika .... yaani Tanzania, umaskini uko chini kuliko South Africa. Duh, sasa ni nini kunatufanya tusiwe kwenye uchumi wa kati ....!!?

Hivi Watanzania wamejifunzia wapi kusifia kiasi hiki ... Yaani watu wanapopewa jukwaa ni mwendo wa kusifia mpaka aibu. Sijui akina Mwinyi, Mkapa na JK wanajisikiaje wanapoalikwa kwenye hafra za Mheshimiwa. Ninekuwa ni mimi ningekuwa nawambia leo sikuamka vizuri ili kukwepa ....!!
Tunadanganya mpaka Shetani anatamani kufuta ile Amri ya 9 kwenye Biblia ambayo inasema "Usiseme Uwongo"
 
Back
Top Bottom