Dkt. Albina Chuwa, Kauli yako kuhusu kupungua kwa umaskini ni kejeli kwa Watanzania

Dkt. Albina Chuwa, Kauli yako kuhusu kupungua kwa umaskini ni kejeli kwa Watanzania

Omba ABC za uchumi kutoka kwa wachumi wakueleze vipimo/viashiria vya kupungua umasikini ni vipi ,hivyo ulivyotaja hata kimoja hakihusiki.

Nakupa mwangaza tu:
1. Kuongozeka kwa pato ghafi la taifa yaani Gross Domestic Product(GDP)

2. Ukuaji wa sekta isiyo rasmi yaani ujasiriamali

3. Uzalishaji viwandani na mashambani kuongezeka. Takwimu zinajieleza.
Acheni utapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunadanganya mpaka Shetani anatamani kufuta ile Amri ya 9 kwenye Biblia ambayo inasema "Usiseme Uwongo"
Tatizo CCM wao bado wako kwenye siasa zao za Ujima sijui Ujamaa... Siasa za North Korea.

Kama Umaskini unapungua si Watoe pia data za unemployment. Unemployment ni indicator kubwa sana na hali nzuri ya maisha ya raia. Ndiyo maana Trump yuko busy na hiyo indicator. Sasa ikija kwetu wa nazungumzia maeneo wanayotaka wao tu.
 
Msiwalaumu wenzenu wajamani. Vyeo vitamu ati....
Amesema Dkt Albina Chuwa Mkurugenzi wa Takwimu. ameyaongea juzi tarehe 17/ 02/ 2020, Ninamnukuu;

“Hali ya umaskini wa kipato hapa nchini Mwaka 1991-92 ulikuwa Asilimia 39, 2007 umaskini ulikuwa asilimia 34, 2012 Asilimia 28.4 na 2018 hali ya umaskini likuwa 26.4, kasi ya kupungua umaskini hapa nchini inaenda kwa mwendo wa kasi”

Full text iko hapa:
Swali:
Umaskini unapungua vipi wakati soko la bidhaa za nje limekufa? Ajira katika sekta binafsi zinakufa? Serikali imeshindwa kuajiri miaka 5? Mshahara bado watu wanapata aliouacha Kikwete?, Umaskini unapungua kwa maskini vipi? Wapambe mnampotosha Rais.

Wahitimu wako mitaani bila ajira, wakulima wa korosho kule Mtwara wamedhulumiwa pesa zao, wafanyabiashara wanaofunga biashara zao kila uchao, umasikini unapunguaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PhD holder waliobaki nawaamini ni wale wa pale main campus na mazimbu pekee.
 
Chuwa kwanza ulipata karai kwenye chemistry, na statistics. Kuwa Director General ni ngekewa tu. Leo umesahau kuwa na wewe ni third class citizen

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama nchi tulipita kipindi kigumu sana. Kweli Albina Chuwa kwa macho makavu alidanganya ili kumfurahisha Mwendazake
 
Kama nchi tulipita kipindi kigumu sana. Kweli Albina Chuwa kwa macho makavu alidanganya ili kumfurahisha Mwendazake
tumepita pagumu. Chuwa ninayemfahamu UDSM leo anasema sentensi kama hizo. Basi naye aende akasafishwe kaburi la chato kama Polepole alivyoshauriwa
 
Hivi hamuoni mpaka wametunga na sheria kabisa kuhalalisha uongo wao?

Hawa binaadam sio wa kawaida hawa.

Katika hali ya kawaida, baada ya kuweka uongo huo, wataalam mbalimbali wangejitokeza kuuchambua na kuupinga.

Sasa hivi ukijitia mjuaji unaishia kupewa kesi ya uhujumu uchumi.

Hili ndilo taifa wanalojenga hawa wazalendo.
Pia ingekua bora zaidi kama watu au Taasisi huru zisizo za kiserikali nazo kuja na takwimu mbadala kuchallenge hizo takwimu za serikali.
 
Pia ingekua bora zaidi kama watu au Taasisi huru zisizo za kiserikali nazo kuja na takwimu mbadala kuchallenge hizo takwimu za serikali.
Maana ya hizo sheria walizotunga ni kuondoa fursa hiyo ya kuhojiwa juu ya uongo wanaowaambia wananchi.
 
Pia ingekua bora zaidi kama watu au Taasisi huru zisizo za kiserikali nazo kuja na takwimu mbadala kuchallenge hizo takwimu za serikali.
Kuna Sheria ya Takwimu ya mwaka 2019 nadhani inazuia mtu yeyote kuchakata Takwimu bila ruhusa ya Mtakwimu Mkuu wa Taifa, yaani Dr Albina Chuwa
 
Kuna Sheria ya Takwimu ya mwaka 2019 nadhani inazuia mtu yeyote kuchakata Takwimu bila ruhusa ya Mtakwimu Mkuu wa Taifa, yaani Dr Albina Chuwa
Kwaiyo wanazuiya tusipime uongo wao😆😆
 
Kwaiyo wanazuiya tusipime uongo wao😆😆
Yes. Hiyo ni Moja kati ya Sheria zaidi ya 10 ambazo zilitengenezwa kwa mfumo wa miscellaneous amendment kati ya mwaka 2015-20 ili kuifanya Tanzania ya Mwendazake full dictatorial state
 
Back
Top Bottom